Wananchi Katika Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga wametakiwa kulinda na kutunza Miundombinu ya Maji kwa kuwa Serikali inatumia gharama kubwa kusogeza huduma ya maji kwa wananchi.
Wito huo umetolewa leo na Waziri wa Maji Mhe.Jumaa Aweso katika usinduzi wa kupanua mradi wa mtandao wa Maji Kijiji la Malenge kata ya Isagehe ambapo amesema, ni haki ya Wananchi kupata maji lakini ni wajibu wao kutunza miundombinu hiyo na kulipa gharama ya matumizi kwakuwa Maji ni huduma sio biashara.
Katika hatua nyingine Aweso amewataka watumishi wa mamlaka ya maji safi na mazingira Wilaya ya Kahama kuboresha utoaji wa huduma kwa wateja ikiwemo kumshirikisha mteja katika usomaji wa Mita za maji ambapo hii imekuwa kero kwa wananchi.
Nae Mbunge wa jimbo la Kahama Mjini Jumanne Kishimba na baadhi ya wananchi Ally Rashidi Na Hawa Masanja wameishukuru Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha za mradi huo kwakua itasaidia kuondoa kero ya ukosefu wa maji kwa wananchi wa kata hiyo ambapo awali walikuwa wanatumia muda mrefu kupata maji.
kwa upande wake Meneja wa mamlaka ya maji safi na mazingira wilaya ya Kahama KUWASA Allen Marwa ameahidi yeye na watumishi wa mamlaka hiyo kuendelea kitoa huduma bora na Maji ya uhakika kwa wateja ambapo hadi sasa ni wananchi 59 walijiunga na mtandao huo.
Upanuzi wa mradi wa mtandao wa maji umefanyika leo katika kata ya Isagehe ambapo vijiji vya Malange, Bukooba, Kidunyashi na Mpera huku jumla ya wakazi 15000 ndio Wanufaika wa mradi huo wenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 900.
0 Comments