TANGAZO

TANGAZO

BEI YA DIZELI, PETROLI YAZIDI KUPAA



Na Mwandishi wetu.

MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetangaza bei mpya za mafuta zitakazoanza kutumika kuanzia leo Jumatano, Oktoba 7, 2026, huku bei za petroli, dizeli na mafuta ya taa zikiongezeka ikilinganishwa na mwezi Septemba 2026.

Kwa mujibu wa taarifa ya EWURA, bei mpya za mafuta zitaanza kutumika kuanzia leo Jumatano, Oktoba 7, 2026 saa 6 usiku.

Kwa bei za rejareja kwa Dar es salaam, petroli imefikia shilingi 4,057 kwa lita, dizeli shilingi 4,086 na mafuta ya taa shilingi 4,067 na Tanga, petroli itauzwa kwa shilingi 4,123, dizeli  shilingi4,152 na mafuta ya taa shilingi 4,133 kwa lita, huku Mtwara petroli ikiwa shilingi ,170, dizeli Sh 4,199 na mafuta ya taa shilingi 4,180 kwa lita.

MWISHO. 







Post a Comment

0 Comments