
Ngayiwa amesema kwa kufanya hivyo kunahatarisha afya zao na kusababisha familia kupoteza wapendwa wao.
Ameyasema hayo wakati akitoa salamu za rambirambi kwa familia ya mfanyabiashara Daudi Shumbi katika kata ya Kagongwa kilichotokea sptemba 28, 2026.
"Niwaombe wananchi tuwasikilize wataalamu wetu, na unapogundua afya yako haipo vizuri tusikimbilie kunywa dawa, tukapime tupatiwe ushauri sahihi wa matumizi ya dawa kulingana na ugonjwa na tiba inayostahili" Amesema Ngayiwa
Mganga mfawidhi kituo cha afya Kagongwa Dk Godfrey Mwaitalako amesema kumekuwepo na wimbi kubwa la wajasiriamali wa dawa za asili zinazotembezwa mtaani ambazo wananhi wanazitumia kiholela hali inayowasababishia madhara ikiwemo vifo.
"Inatakiwa tuchukue tahadhari kubwa dhidi ya dawa tunazotumia, ni kweli kwamba dawa zote tunazotumia kwa kiwango kikubwa zinatokana na mitishamba lakini zimechunguzwa na kuthibitishwa kuwa salama kwa binadamu." Amesema Dk Godfrey na kuongeza
"Serikali ilitambua kuwa kila mwananchi ana mila na desturi anazozifuata ambazo wakati mwingine zinawalazimu kutumia dawa za asili, hivyo ikaweka utaratibu wa kutumia dawa hizo, ikaja na suala la tiba mbadala ambazo nazo zimethibitishwa na wapo wataalamu waliotambuliwa na kupewa usajili."
"Tusichukue dawa kiholela, kama ni za hospitali tupewe na wataalamu na kama ni tiba mbadala bai pia tupewe na wataalamu."
Akizungumza kwa niaba ya familia diwani wa kata ya Segese jimbo la Msalala Patrick Mahona, amewashukru madaktari katika hospitali ya Manispaa ya Kahama kwa jitihada kubwa walizofanya kuokoa uhai wa marehemu bila mafanikio.
Amesema "Naishukuru sana hospitali ya Manispaa ya Kahama kwa jitihada walizotuonyesha tangu tunafika mpaka kutupatia usafiri kwa ajili ya kumhamisha mgonjwa wetu kwenda Shinyanga, lakini ni mapenzi ya Mungu yametimia."
Mganga mfawidhi kituo cha Afya Kagongwa Dk Godfrey Mwaitalako akitoa salamu za rambirambi.
Diwani wa kata ya Segese jimbo la Msalala Patrick Mahona akitoa shukrani kwa niaba ya familia kwa hospitali ya Manispaa ya Kahama kwa juhudi na ushirikiano walioutoa kwa marehemu kipindi cha ugonjwa mpaka mauti yanamkuta.
Jeneza lililobeba mwili wa mfanyabiashara Daudi Shumbi aliyefariki dunia septemba 28, 2026, likiwa mbele ya waombolezaji kwa ajili ya ibada ya maziko.
Waombolezaji wakiwa msibani kata ya Kagongwa Manispaa ya Kahama.






0 Comments