TANGAZO

TANGAZO

Video : WANANCHI WAMJIA JUU MBUNGE NGAYIWA KUFANYA MIKUTANO BILA WATAALAMU, WADAI NI SIASA



Mwananchi wa mtaa wa Mayila, kata ya Nyihogo Halmashauri ya Manispaa ya Kahama Richard Audax akizungumza kwenye mkuatano wa hadhara wa mbunge Ngayiwa wa kusikliza na kutatua kero za wananchi.


Video 👇


 

Siku chache baada ya Mbunge wa Kahama Mjini, Mhe. Benjamin Ngayiwa, kulalamikia baadhi ya wataalamu wa Idara za serikali kutohudhuria mikutano ya kusikiliza na kutatua kero za wananhi, leo wananchi wa Nyihogo, mtaa wa Mayila wamemjia juu wakieleza kuwa kitendo hicho ni kuendelea kuwafanyia siasa.

 

Mwananchi Richard Audax mkazi wa mtaa huo amemtaka mbunge kangalia suala la mikutano ya kero za wananchi na majibu yatolewe na wataalamu badala ya mbunge mwenyewe ambaye wanaamini kazi yake ni kusimamia utekelezaji.


 Hoja hiyo imeibuliwa kwenye Mkutano wa Hadhara Kata ya Nyihogo Manispaa ya Kahama Mkoani Shinyanga uliolenga kusikiliza na kutatua changamoto za wananchi.


"Inatakiwa unapoondoka katika msafara wako, hakikisha unaondoka na wakuu wa idara, ili tukihoji maji anajibu, tukihoji kuhusu umeme anatujibu, barabara tujibiwe na wataalamu, wewe ni siasa tu hapa?" Amesema Audax
















Post a Comment

0 Comments