TANGAZO

TANGAZO

MUME ATUHUMIWA KUMCHINJA MKEWE NA KUTUPA VIUNGO MTONI



Polisi Wilayani Makete, Mkoa wa Njombe, inamshikilia mkazi wa wilaya hiyo Juma Kyando (36), kwa tuhuma za mauaji ya mkewe Tumaini Luvanda (35), ambapo inadaiwa mtuhumiwa alimchinja na kutenganisha kichwa na kiwiliwili.

Taarifa ya awali inasema kuwa baada ya kumchinja, mtuhumiwa aliukata mwili huo vipande vipande na kisha kutupa baadhi ya viungo kwenye mto, huku vingine akivitupa jirani na nyumba yake eneo la Kabinda lililopo wilayani humo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe, Mahamoud Banga amethibitisha kutokea kwa mauaji hayo na kudai kuwa kesho atatolea ufafanuzi zaidi.

"Tukio kweli limetokea lakini kesho nitalitolea ufafanuzi nitakapozungumza na wanahabari," amesema Kamanda Banga.

Post a Comment

0 Comments