TANGAZO

TANGAZO

MADENI YADAIWA KUSABABISHA KIFO CHA DEREVA PIKIPIKI KAHAMA

 

Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Valley Thabit ambaye ni dereva wa pikipiki (bodaboda) mkazi wa Nyihogo ameuawa kwa kunyongwa na kamba na watu waliomchukua kama wateja katika Kijiji cha Penzi kata ya Mondo Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga.

Akizungumza kwa niaba ya ndugu, kaka wa marehemu Apolinali Penda amesema tukio hilo limetokea januari 3 mwaka huu, majira ya usiku, ambapo watu hao baada ya kutekeleza mauaji hayo walikimbia licha ya juhudi za wananchi eneo hilo kuwadhibiti kutofanikiwa.

“Nilipigiwa Simu na Mke wangu akiniarifu juu ya mdogo wangu kuuawa na nilipofika nikaanza ufuatiliaji hadi polisi, lakini kwa mujibu wa shuhuda anasema kuna purukushani eneo la tukio ambapo mdogo wangu alisikika akidai wamwachie uhai atawalipa pesa zao, akaenda kuita wananchi, walipofika wahusika waliotekeleza mauaji hayo walikimbia ambapo ilikutwa kamba inayoonesha ndo ilitumika kumnyonga, jitihada zinaendelea kuwabaini waliohusika nak ama familia tunajiandaa kusafirisha mwili kwaajili ya mazishi”.

Juhudi za kulitafuta Jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga ili kutolea taarifa rasmi juu ya tukio hilo bado zinaendelea.............

Post a Comment

0 Comments