TANGAZO

TANGAZO

WENYEVITI EPUKENI MIGOGORO ISIYO YA LAZIMA - KISHIMBA

Wenyeviti wa mitaa na Vijiji katika Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga, wametakiwa kudumisha uhusiano mzuri na wananchi wanao watawala ili kuleta maendeleo.

Wito huo umetolewa leo na Mbunge wa Jimbo la Kahama Mjini Jumanne Kishimba katika kikao na Wenyeviti wa mitaa na Vijiji kwenye ukumbi wa Idara ya maji Kahama kwa lengo la kujadiri changamoto na maendeleo ya miradi mbalimbalimbali ya maendeleo.

Kishimba amesema ni jukumu la kila mwenyekiti kuwa na uhusiano mzuri na wananchi wake ikiwa ni pamoja na kutetea huduma za kijamii, na kushughulikia kero mbalimbali kama migogoro ya ardhi, Michango isiyo na tija hali inayokwamisha utekeleza wa miradi ya maendeleo.

"Ndugu zangu niwaombe sana, jengeni mahusiano mazuri na Wananchi, epukeni migogoro isiyo ya lazima, shirikisheni Wananchi vizuri lakini pia muwe na mahusiano mazuri kati yenu na mabalozi wa mitaa ,madiwani pamoja na watumishi wa serikali wakiwemo watendaji ili nguvu hizo zote ziwe na tija kwa maendeleo ya wananchi na mitaa yenu"

Katika hatua nyingine Kishimba amewataka wenyeviti hao kuongeza ubunifu wa miradi katika mitaa na Vijiji vyao hali itakayosaidia kukua kwa mitaa kiuchumi ambapo Serikali inafanyia kazi miradi yote inayotakiwa kukamilishwa ikiwemo kupaua maboma ya madarasa, Zahanati na nyumba za watumishi.

Wakizungumza kwa niaba ya Wenyeviti hao Anania Miligo Mwenyekiti wa Mtaa wa Majengo na Patroba Privatus Mwenyekiti mtaa wa Sokola wamemshukuru Mbunge kwa kukutana nao na kuahidi kutatua kero za wananchi katika kuleta maendeleo

Post a Comment

0 Comments