Watu watano wamebainika kuwa na Ugonjwa wa Kipindupindu Katika Mji Mdogo wa Kagongwa Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo watu wengie 452 wanaendelea kufuatiliwa baada ya kuchangamana nao na wengine 13 wakiwa wamelazwa katika Kituo cha Afya Mwendakulima kwa ajili ya Matibabu.
Kufuatia taarifa hiyo mkuu wa Wilaya ya Kahama Mboni Mhita ameelezea hatua zilizochukuliwa na Serikali, huku Mganga mkuu wa Manispaa ya Kahama Dkt Shani Mdami akielezea hali ya Wagongwa.
Baadhi ya Wakazi wa Mji mdogo wa Kagongwa akiwemo Michael Shija ambaye ni Mwenyekiti wa Mtaa wa Kagongwa ameelezea kilichosabisha wakabaini kuwepo kwa wagonjwa hao ambapo ilianzia kwa mtoto ambaye aliugua kwa kuharisha na kutapika saana na watu waliokuwepo kwenye msiba ule wakaanza kuhara baada ya siku mbili akiwemo mkuu wa Nzengo ambaye naye alifariki ndipo hatua nyingine za ufuatiliaji zikafanyika.
Restuta John ni mmoja wa wakazi wa Kagongwa amesema kufuatia watu wengi kuhara watu wameanza kuchukua tahadhari ikiwemo kunawa Maji kabla ya kula chochote.
0 Comments