
Mvua ya Mawe na Upepo imeleta
maafa katika Kijiji cha Ibanza Kata ya Mwamala wilayani Shinyanga ambapo nyumba
51 zimeanguka na kusababisha wananchi kukosa makazi, pamoja na kuathiri
mashamba na mifugo.
Tukio hilo limetokea majira ya saa 9 usiku wa kuamkia Desemba 06 mwaka huu 202usiku wa kuamkia Desemba 6,2023 majira ya saa 9 usiku.
Mmoja wa waathirika wa tukio hilo Jilala Dutu, amesema mvua ilianza kunyesha majira hayo ya usiku huku wakiwa wamelala, lakini ghafla walisikia mabati yakibebwa na upepo na kutupwa pembeni na nyumba yao, na wakati huo huo nyumba ikianguka kwa ndani na kujeruhi mtoto na Mama Mkwe wake.


Akieleza maafa yaliyotokana na mvua hizo Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Simon Berege, amesema nyumba 51 zimeanguka, mashamba ya mahindi Hekari 10 yameathirika, kuku 20 wamekufa na mbuzi mmoja amekufa na hakuna kifo, na Bibi ambaye amevunjika Mguu anapatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme aliyefika eneo la tukio, ametoa pole kwa waathirika wote wa mvua hiyo, huku akibainisha kuwa kwa wananchi ambao wote wameumia Serikali itagharamikia matibabu yao.






0 Comments