Msemaji Mkuu wa Serikali, Mobhare Matinyi , amesema wamefanikiwa kupata miili minne ya wahanga wa maporomoko ya matope kutoka Mlima Hanang’ mkoani manyara na kufanya idadi ya vifo kufikia 69.
Matinyi ameyasema hayo leo Desemba 6, mwaka huu 2023
wakati akizungumza na waandishi wa habari wilayani Hanang' wakati zoezi la
maokozi likiendelea, ambapo miili iliyopatikana wawili ni wanawake na
wawili ni wanaume.
hata hivyo kati ya majeruhi 117 walioripotiwa
awali katika ajali hiyo, Matinyi alisema wapo walioruhusiwa kutoka hospitalini,
mmoja alifariki hivyo idadi ya majeruhi hivi sasa ni 45.
0 Comments