Waziri wa Maji Jumaa Aweso amewahakikishia wananchi upatikanaji wa huduma ya maji katika maeneo ya vijiji na kata zilizoathiriwa na maporomoko ya matope kutoka Mlima Hanang’ yaliyosababisha miundombinu ya maji kuharibiwa na kusababisha madhara ikiwemo vifo, majeruhi na uharibifu wa mali.
Waziri Aweso ameeleza hayo wakati akizunguka
katika maeneo hayo na kujionea hali ya upatikanaji huduma ya maji na jitihada
ya kurejesha miundombinu ya Maji katika mji wa Katesh na maeneo mengine.
Amesema Wizara ya Maji imechukua hatua ya dharura
kwa kuweka matenki ya maji 30, yaliyosambazwa katika makambi, vituo vya huduma
za afya na maeneo ya vijiji vyote yaliyoathirika hasa Kata za Gendabi, Jorodom,
Ganana, Katesh, Mogitu na Dumbeta.
Aidha, Waziri Aweso amekabidhi matenki ya maji 30
kwa madiwani na kuhakikisha yanaletwa mabomba ya maji matano yanayopeleka maji
katika matenki na kuwafikishia wananchi huduma ya majisafi na salama muda wote.
Waziri Aweso amekagua na kujionea mitambo ya
kuchimba kisima cha maji ambayo tayari imeanza kazi ambapo itasaidia kuongeza
maji katika vyanzo ambavyo havijaaribiwa na maafa hayo.
0 Comments