RAIS Samia Suluhu Hassan amesema serikali kupitia balozi zake na majukwaa mbalimbali yataendelea na jitihada za kufungua masoko ya zao la karafuu ili kuongeza uuzaji wa zao hilo nje ya nchi.
Kiongozi huyo wa nchi ametoa kauli hiyo leo alipozungumza na wananchi katika tukio la azinduzi wa jengo la Kitega Uchumi la Zanzibar State Trade Cooperation – Pemba visiwani Zanzibar.
Rais Samia amesema mahitaji ya soko la karafuu kimataifa bado kubwa, hivyo amewataka wahusika wa uzalishaji wa zao hilo kuongeza jitihada katika uzalishaji wa zao hilo.
Amesema wakati taifa linalenga kuongeza kiwango cha uzalishaji, shabaha ibaki katika kuongeza tija ya uzalishaji kwa kila ekari.
“Angalizo langu kwenye hili, tunapotafuta njia za kisanyansi kuongeza tija ya uzalishaji tusishushe hadhi na ubora wa karufuu yetu.
Tuongeze uzalishaji lakini ubora wa karufuu yetu ibaki vile vile, tunaweza tukapata watalamu wa sayansi wakatuongezea uzalishaji lakini hadhi ya karufuu yetu ikashuka”.Amesema Rais Samia.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa na Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar Mhe. Omar Said Shaabani pamoja na viongozi mbalimbali wakati akikata utepe kuashiria ufunguzi wa Jengo la Kitega Uchumi la Shirika la Biashara la Taifa Zanzibar (ZSTC) lililopo Chakechake Pemba tarehe 09 Januari, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akivuta kitambaa pamoja na Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar Mhe. Omar Said Shaabani kuashiria ufunguzi wa Jengo la Kitega Uchumi la Shirika la Biashara la Taifa Zanzibar (ZSTC) lililopo Chakechake Pemba tarehe 09 Januari, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Mkurugenzi Mwendeshaji wa Shirika la Taifa la Biashara Zanzibar (ZSTC) Soud Said Ally kuhusu Kituo cha kupimia Karafuu kilichopo katika jengo hilo la Kitega Uchumi la ZSTC Pemba tarehe 09 Januari, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na viongozi mbalimbali mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Pemba tarehe 09 Januari, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na viongozi mbalimbali mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Pemba tarehe 09 Januari, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na viongozi mbalimbali mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Pemba kwa ajili ya ziara ya kikazi tarehe 09 Januari, 2024.
Shamrashamra za ufunguzi wa Jengo la Kitega Uchumi la Shirika la Biashara la Taifa Zanzibar (ZSTC) Karafuu House, Chake Chake Kisiwani Pemba tarehe 09 Januari, 2024.
0 Comments