TANGAZO

TANGAZO

HUDUMA BORA ZA MAWASILIANO NI MUHIMU KWA KUWA NI KICHOCHEO KATIKA KULETA MAENDELEO YA JAMII-MAJALIWA


WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan itaendelea kuhakikisha kuwa wananchi wote wa Tanzania wanapata haki ya kikatiba ya kupata habari kama ilivyoainishwa katika ibara 18 (2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Majaliwa amenukuu sehemu ya Katiba inayozungumzia haki ya wananchi kupata habari inayosema: “Kila raia anayo haki ya kupewa taarifa wakati wote kuhusu matukio mbalimbali nchini na duniani kote ambayo ni muhimu kwa maisha na shughuli za wananchi na pia juu ya masuala muhimu kwa jamii”.

Alisema hayo wakati akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Ruangwa baada ya kuzindua studio za Redio Jamii- Ruangwa katika ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa, Lindi. Majaliwa alisema huduma bora za mawasiliano ni muhimu kwa kuwa ni kichocheo katika kuleta maendeleo ya jamii na nchi nzima kwa ujumla.

Alisema ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ya Mwaka 2020-2025; Ibara ya 125 (a) imeielekeza serikali kuendelea kutekeleza Sheria ya Huduma za Habari Na 12 ya mwaka 2016 ili kuhakikisha kuwa wananchi wanapata taarifa sahihi kwa urahisi zaidi na kwa wakati.

Majaliwa alisema kuwa uzinduzi wa kituo hicho ni sehemu ya utekelezaji wa matakwa ya Ilani ambayo imedhamiria kuhakikisha kuwa sekta ya habari inaboreshwa ili kuwaongezea wananchi fursa ya kupata habari kwa kuongeza wigo wa upashanaji wa habari.

Post a Comment

0 Comments