Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan, amesema wataalam wa serikali, tayari wametenga eneo ambalo litatumika kuwahamisha waathirika wa maporomoko ya tope, Hanang mkoani manyara ambapo itawaunga mkono katika ujenzi wa makazi mapya ya kudumu.
Rais Samia aliyasema hayo wakati alipozuru eneo la janga hilo katika mji wa Katesh wilayani Hanang kuwapa pole na kuwajulia hali waathirika wa janga hilo, lililosababisha vifo vya watu 76 na kuwajeruhi wengine zaidi ya 100 ambao wanapata matibabu hospitalini.
Pia alizitaka taasisi za serikali kuwa na utaratibu wa kuchunguza kwa makini majanga ya asili kabla hayajatokea na kuchukua tahadhari ili kuepusha madhara kama yaliyotokea Hanang, huku akisisitiza wataalamu kuendelea kujiimarisha uwezo wa kuweza kubaini mapema viashiria au majanga u hatari za namna hiyo.
''Serikali sasa tunaongeza uwezo wetu wa kukabiliana na maafa kwa vifaa na pia utaalamu'', aliongeza.
Rais Dkt Samia amesema serikali ilichukulie janga la Hanang liwe funzo kwao na wajipange mapema kuwa na taarifa zote ili kuepuka majanga hayo yasiwakute wananchi wakiwa hawajajipanga.
''Wataalamu wamepata eneo la kuwahamishi wahanga, serikali itahakikisha inashirikiana nao ili kufanya hilo kwa haraka''. amesema Rais Samia.
Kuhusu janga hilo Rais Samia amesema ameagiza ufanyike uchunguzi kuhusu kiini na tarifa za kina zipatikane haraka na kuelewa kilichotokea ili kudhibiti athari za mafuriko katika siku zijazo .
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan akizungumza na baadhi ya majeruhi aliowatembelea leo kuwajulia hali katika Hospitali
ya Tumaini Wilayani Hanang na kuwapa pole pamoja na kuwatakia afya njema.
0 Comments