.jpeg)
Wadau wa maendeleo katika Halmashauri ya Ushetu
mkoani Shinyanga, wameombwa kuunganisha nguvu ili kupata shule ya Watoto wenye
mahitaji maalumu ili kusaidia kundi hilo kutimiza ndoto zao.
Ombi hilo limetolewa na mbunge wa jimbo la Ushetu Emanuel Cherehan, aliyekuwa mgeni rasmi katika kongamano la kupinga ukatili, lililofanyika katika Halmashauri hiyo, na kuwakutanisha wadau mbalimbali wa kupinga ukatili.
"Lakini pia kitu ambacho natamani tukipate ni shule ya wenye uhitaji, uwezo huo tunao, tuna wadau wa kutosha, mimi mwenyewe ni mdau, wanunuzi wa tumbaku ni wadau, madiwani ni wadau, kwa nini tusiwe na eneo tulitenge tupate shule yao?" Alieleza Mbunge Cherehan na kuongeza kuwa
"Kwa upande wa halmashauri ya Ushetu hii ni changamoto kubwa, watu wenye ualbino wanatamani kusoma lakini waende wapi, vipofu wanahitaji kusoma waende wapi, na napenda hii shule ijengwe katika makao makuu ya Halmashauri_Nyamilangano" Alisisitiza
Katika hatua nyingine Mhe. Cherehan amesema wanafunzi wa kike katika halmashauri hiyo wanakabiliw na changamoto ya maeneo salama ya kujistiri wanapokuwa katika siku zao za hedhi, huku akisisitiza kuwa nao ni ukatili kwao.
"sio walemavu tu Mkurugenzi, kuna wanafunzi wetu wananyanyasika sana wanapokuwa katika siku zao, hawana hata eneo la kujistiri, na hata kama lipo halipo katika hali ya wao kujiachia" Alisisitiza Cherehan
.jpeg)
.jpeg)

.jpeg)
.jpeg)

.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)
0 Comments