Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mboni Mhita, akikabidhi mfano wa hundi ya Sh2,167,520,000 kwa ajili ya vikundi 96 vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu kupitia mpango wa mikopo ya asilimia 10 ya mapato ya ndani ya Halmashauri ya Manispaa ya Kahama, Novemba 5, 2026.
Picha na Kadama Malunde

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mboni Mhita, akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi mikopo yenye thamani ya Sh2,167,520,000 kwa vikundi 96 vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu kupitia mpango wa mikopo ya asilimia 10 ya mapato ya ndani ya Halmashauri ya Manispaa ya Kahama, Novemba 5, 2026.

Mmoja wa wanufaika wa mikopo hiyo, Adam Mohamed Mlasi, akitoa neno la shukrani kwa Serikali na Halmashauri ya Manispaa ya Kahama kwa kuwawezesha kupata mikopo kupitia mpango wa asilimia 10 ya mapato ya ndani ya Halmashauri, Novemba 5, 2026.
Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Francis Mlacha, akizungumza wakati wa hafla ya utoaji wa mikopo yenye thamani ya Sh2.16 bilioni kwa vikundi 96 vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu kupitia mpango wa mikopo ya asilimia 10 ya mapato ya ndani ya Halmashauri ya Manispaa ya Kahama, Novemba 5, 2026.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kahama, Masudi Kibetu, akitoa taarifa ya utoaji wa mikopo ya asilimia 10 ya mapato ya ndani ya Halmashauri, akieleza kiasi cha fedha kilichotolewa, idadi ya vikundi vilivyonufaika na mipango ya kuendelea kuwawezesha wanawake, vijana na watu wenye ulemavu, Novemba 5, 2026.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Manispaa ya Kahama, Thomas Muyonga, akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi mikopo yenye thamani ya Sh2.16 bilioni kwa vikundi 96 vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu, kupitia mpango wa mikopo ya asilimia 10 ya mapato ya ndani ya Halmashauri ya Manispaa ya Kahama, Novemba 5, 2026.
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Kahama, Mataluma Kaniki, akizungumza wakati wa hafla ya utoaji wa mikopo ya Sh2.16 bilioni kwa vikundi 96 vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu, akieleza dhamira ya Manispaa hiyo kuongeza mikopo hadi kufikia Sh4 bilioni ifikapo Juni 2027, Novemba 5, 2026.
Na Neema Nkumbi, Kahama
Halmashauri ya Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga imetoa mikopo yenye thamani ya Sh2,167,520,000 kwa vikundi 96 vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu kupitia mpango wa mikopo ya asilimia 10 ya mapato ya ndani ya Halmashauri, huku Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mboni Mhita, akitaka wanufaika waunganishwe na fursa za zabuni za Serikali ili kukuza biashara zao na kuongeza uwezo wa kurejesha mikopo hiyo.
Mikopo hiyo imetolewa Novemba 5, 2026, katika hafla iliyofanyika Manispaa ya Kahama na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali, Chama cha Mapinduzi (CCM), vyama vingine vya siasa, madiwani pamoja na wanufaika.
Kwa mujibu wa takwimu zilizowasilishwa katika hafla hiyo, vikundi 46 vya wanawake vimepatiwa Sh708,520,000, vikundi 45 vya vijana vimepata Sh1,428,000,000, huku vikundi vitano vya watu wenye ulemavu vikikabidhiwa Sh31,000,000.
Akizungumza katika hafla hiyo, Mhita amesema mpango wa mikopo ya asilimia 10 ni sehemu ya utekelezaji wa maelekezo ya Rais Samia Suluhu Hassan yenye lengo la kuwawezesha wanawake, vijana na watu wenye ulemavu kiuchumi kwa kuwapatia mitaji isiyo na riba.
Amesema wanufaika wanapaswa kuelewa kuwa fedha hizo siyo msaada wa bure, bali ni mikopo inayopaswa kutumika kuzalisha na kurejeshwa kwa wakati ili kuwawezesha wananchi wengine kupata fursa kama hiyo.
“Wale mliokopeshwa, hizi fedha siyo fedha za msaada. Ni mikopo isiyo na riba ambayo inapaswa kurejeshwa. Utaratibu wake ni Kopa, zalisha na rudisha. Msitumie fedha hizi kwa matumizi yasiyokusudiwa, bali zitumieni kujijenga kiuchumi,” amesema Mhita.
Amesisitiza kuwa utoaji wa mikopo pekee hautoshi kuhakikisha wanufaika wanafanikiwa, hivyo ni muhimu Halmashauri kuhakikisha wanapata elimu ya ujasiriamali, ushauri wa kitaalamu na fursa za masoko zitakazowasaidia kukuza biashara zao.
Katika kuhakikisha wanufaika wanapata masoko ya uhakika, Mhita ameitaka Halmashauri kuwaunganisha wajasiriamali hao na fursa za zabuni zinazotolewa na Serikali, ili waweze kushiriki katika uzalishaji wa bidhaa na utoaji wa huduma zinazohitajika katika miradi mbalimbali ya maendeleo.
Ametolea mfano vijana wanaoweza kuzalisha bidhaa na vifaa vinavyohitajika katika miradi ya Serikali, akieleza kuwa badala ya Halmashauri kununua bidhaa hizo kutoka kwa wazalishaji wa nje, ni vyema kuwapa fursa wajasiriamali wa ndani ambao tayari wamewezeshwa kupitia mikopo hiyo.
Amesema hatua hiyo itawasaidia wanufaika kupata masoko, kuongeza kipato na kuimarisha uwezo wao wa kurejesha mikopo, sambamba na kujenga historia nzuri ya mikopo itakayowawezesha kupata mitaji mikubwa zaidi kutoka taasisi za fedha.
Akizungumzia umuhimu wa amani na usalama katika maendeleo ya kiuchumi, Mhita amesema mikopo hiyo ni miongoni mwa fursa zinazowezeshwa na mazingira ya amani yaliyopo nchini, hivyo amewataka wananchi kutokubali kushawishiwa katika vitendo vinavyoweza kuhatarisha amani.
“Mikopo hii imetolewa kutokana na kwamba nchi yetu ina amani na usalama. Tusikubali kuyumbishwa na watu wasioitakia mema nchi yetu wala kudanganyika. Tuendelee kutunza amani ya nchi yetu. Anayekupenda anakupa mchongo wa kujiinua kiuchumi, lakini asiyekupa mchongo wa kujiinua kiuchumi huyo ni mnafiki na mzandiki,” amesema Mhita.
Aidha, amewataka viongozi wa Halmashauri na wataalamu wa maendeleo ya jamii kuhakikisha wanufaika wanapatiwa elimu ya usimamizi wa fedha, ujasiriamali na uendeshaji wa biashara ili mikopo hiyo itumike kwa malengo yaliyokusudiwa na kuleta matokeo chanya.
Amesema mafanikio ya mpango huo yanahitaji usimamizi na ufuatiliaji wa karibu wa miradi pamoja na urejeshaji wa mikopo kwa wakati, ili fedha hizo ziendelee kuzunguka na kuwawezesha wananchi wengine.
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Dkt. Francis Mlacha, amewataka wanufaika kutumia fedha walizopatiwa kwa shughuli za kiuchumi walizoziainisha katika maombi yao badala ya kuelekeza mikopo hiyo kwenye matumizi mengine.
Amesema mikopo hiyo haina riba na inapaswa kuchukuliwa kama mbegu ya kujenga msingi wa kujitegemea kiuchumi.
“Mkopo huu ni kama mbegu na hauna riba. Kwa hiyo, mkopo huu utumieni kama mbegu itakayochipua na kuwasaidia kujikwamua kiuchumi na kutokuwa tegemezi,” amesema Dkt. Mlacha.
Ameongeza kuwa wanufaika wanapaswa kufanya kazi kwa bidii, kusimamia vizuri miradi yao na kuhakikisha wanarejesha mikopo kwa wakati ili wananchi wengine nao wapate fursa ya kunufaika na mpango huo.
Pia amewataka wananchi kuendelea kudumisha amani, utulivu na mshikamano akieleza kuwa mazingira hayo ni muhimu katika kukuza uchumi na kuharakisha utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Naye Mkurugenzi wa Manispaa ya Kahama, Masudi Kibetu, amesema Halmashauri hiyo ilianza kutoa mikopo kwa utaratibu mpya wa asilimia 10 Januari 2025 na kwamba hadi Oktoba 2026 ilikuwa imetoa jumla ya Sh6,377,691,500 kwa vikundi 335.
Amesema mikopo hiyo imeelekezwa katika shughuli mbalimbali za kiuchumi kulingana na mahitaji na maombi ya wanufaika, zikiwemo biashara za usafirishaji kwa kutumia pikipiki na bajaji, ununuzi wa magari, uchakataji na usindikaji wa samaki, ufugaji wa kuku, maduka, biashara ya vipuri vya magari pamoja na vifaa vya ujenzi (hardware).
Kibetu amesema kwa mwaka wa fedha 2026/2027, Manispaa ya Kahama imetenga Sh2 bilioni kutoka mapato ya ndani na marejesho ya mikopo kwa ajili ya kuendelea kuwawezesha wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.
Ameishukuru Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwezesha utekelezaji wa mpango huo na kuwataka wanufaika kutumia fursa waliyoipata kuimarisha shughuli zao za kiuchumi.
Kwa upande wake, Meya wa Manispaa ya Kahama, Mataluma Kaniki, amesema Baraza la Madiwani kwa kushirikiana na wataalamu wa Halmashauri limejipanga kuhakikisha ifikapo Juni 2027 Manispaa hiyo inatoa mikopo isiyopungua Sh4 bilioni.
“Tunajipanga vizuri kuhakikisha ifikapo Juni mwaka 2027, Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa utakuwa tena hapa kuja kukabidhi hundi isiyopungua Sh4 bilioni au zaidi,” amesema Kaniki.
Amesema Manispaa inaendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo, ikiwemo ujenzi wa jengo la Mama na Mtoto katika Hospitali ya Manispaa ya Kahama, huku akimshukuru Rais kwa fedha zinazotolewa kwa ajili ya kuboresha huduma na maisha ya wananchi.
Naye Mwenyekiti wa CCM wa Manispaa ya Kahama, Thomas Muyonga, amewapongeza Meya na madiwani kwa kusimamia utekelezaji wa mpango huo, akisema utoaji wa mikopo hiyo ni sehemu ya juhudi za kuwawezesha wananchi kiuchumi.
Muyonga amewataka wanufaika kuzingatia nidhamu ya biashara, kufanya kazi kwa bidii na kutumia fedha walizopatiwa kwa malengo yaliyokusudiwa ili kukuza mitaji na kuboresha maisha yao.
Amesisitiza umuhimu wa wanufaika kurejesha mikopo kwa wakati ili kuhakikisha fedha hizo zinaendelea kuzunguka na kuwafikia wananchi wengine wenye mahitaji.
Utoaji wa mikopo hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa mpango wa Halmashauri wa kutenga asilimia 10 ya mapato ya ndani kwa ajili ya kuwawezesha wanawake, vijana na watu wenye ulemavu kupata mitaji ya kuanzisha na kukuza shughuli za kiuchumi.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mboni Mhita, akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi mikopo yenye thamani ya Sh2,167,520,000 kwa vikundi 96 vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu kupitia mpango wa mikopo ya asilimia 10 ya mapato ya ndani ya Halmashauri ya Manispaa ya Kahama, Novemba 5, 2026

0 Comments