MAKAMU Mwenyekiti wa chama cha ACT Wazalendo Bara, Dorothy Semu Februari 18 2024 amechukua fomu kugombea nafasi ya kiongozi mkuu wa chama hicho, nafasi iliyoachwa wazi na Zitto Kabwe.
Baada ya kuchukua fomu, Semu ametoa hotuba ifuatayo:
Ndugu watanzania
Ndugu viongozi, wanachama, wapenzi na wafuasi wa ACT Wazalendo kipekee wote mlionisindikiza kutoka kila kona kujumuika nami hapa katika tukio hili la kihistoria kwa taasisi yetu.
Huu ni uchaguzi wa tatu tangu kuasisiwa kwa ACT Wazalendo na kwa sasa ni lazima kuwa na KC mpya.
Ndugu wanahabari nimefika hapa, baada ya tafakuri ya kina na uamuzi usio na shaka, utayari wa kuendelea kuwatumikia wana ACT Wazalendo nikiomba ridhaa wanitumetena kutumikia katika nafasi hii ya juu kuliko zote. Nimechukua fomu ya kugombea nafasi ya Kiongozi wa chama.
Dhamira yangu hii ya dhati inaongozwa na mambo matatu.Jambo la kwanza naamini katika uongozi wa pamoja, utumishi wa watu na kuonyesha njia ili kutimiza kwa ukamilifu malengo makubwa ya taasisi kuelekea ndoto ya ACT Wazalendo .
Mmenipima kwenye majukumu mbalimbali mlioniamini kwayo kwa miaka hii nane, baada ya kuwa mtumishi wa umma kwa miaka 17. Nitaje machache, nilipokuwa Katibu Mkuu 2017-2020 nimekivusha chama kwenye mawimbi ukandamizaji wa kidemokrasia, mawimbi ya kufutiwa usajili na hata kwa pamoja kuvunja rekodi za usimamizi wa kifedhana kuwa chama kinachokua kwa kasi kuliko vyote Afrika.
Nikiwa Makamu Mwenyekiti Bara mwaka 2021 nilipewa jukumu jingine la kukaimu Uenyekiti wa chama baada ya kutangulia mbele za haki kwa aliyekuwa mwenyekiti wetu mpendwa Maalim Seif *Mungu amrehemu na kukakikisha anapatikana Mwenyekiti mwingine kwa mfumo wa kidemokrasia kama matakwa ya katiba yetu ya chama.
Mmeniamini kiungozi, nami nimerudisha kwa kuwa mtumishi mwaminimifu, nisiyelega wala kukata tamaa. Ninataka kutumia uzoefu wangu na karama yangu ya uongozi sasa kuongoza jahazi hili la ACT Wazalendo kwenye kushika hatamu za kuongoza taifa hili.
0 Comments