Wabunge Wanawake mkoani Shinyanga wamelaani vikali tukio la vifo vya Mama na mtoto lililotokea katika Hospitali ya Wilaya ya Kahama kwa madai ya kukosa huduma wakati alipokwenda kujifungua.
Mbunge wa viti maalum mkoani humo Dkt Christine Mnzava, amewaambia wanahabari kuwa wanawake mkoani Shinyanga hawatofumbia macho vifo vya uzazi, wakati ambapo serikali inafanya jitihada kubwa za kuimarisha miundombinu ya majengo ya kutolea huduma.
Katika hatua nyingine Dkt Mnzava amewataka wanafamilia Pamoja na jamii kwa ujumla, kuwa wavumilivu wakati ambapo tayari serikali ya wilaya ya Kahama imeunda timu mbili kwa ajili ya kufuatilia tukio hilo.
Hivi karibuni mkuu wa wilaya ya Kahama Mboni Mhita, alieleza kuwa tayari zimeundwa timu mbili kwa ajili ya uchunguzi wa tukio hilo, sambamba na kuwasimamisha kazi watoa huduma 6 waliokuwepo zamu kwa siku husika, na tayari wameanza kuhojiwa na jeshi la polisi wilayani humo.
0 Comments