
Ubovu wa miundombinu ya Barabara katika manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga umetajwa kuchangia pakubwa kukwamisha shughuli za kiuchumi kwa wananchi huku jitihada za dharura zikihitajika kuchukuliwa ili kunusuru hali hiyo.
Hayo yamebainishwa na Mabalozi wa Mashina katika Kikao kilichoandaliwa na Mbunge wa Jimbo la Kahama Mjini Jumanne Kishimba ambaye akitoa mchango wake pia ameomba kuwepo kwa Mawazo ya kipi kifanyike cha dharura kwa Mamlaka na Jamii kwa ujumla.
Akitolea majawabu juu ya changamoto hiyo Meneja TARURA manispaa ya Kahama Shija Mhangale amesema zoezi la urejeshaji wa miundombinu ya Barabara katika hali ya kawaida lilisimama kutokana na uwepo wa Mvua nyingi lakini pia bajeti kutofika kwa wakati huku akiomba ushirikiano kutoka kwa jamii kupitia Mabalozi.
Kikao cha Mabalozi ambao ndiyo wenyeviti wa Mashina katika Kata zote Manispaa ya Kahama ni mwendelezo wa Vikao ambavyo Mbunge jimbo la Kahama mjini Jumanne Kishimba anavifanya kwa viongozi ngazi ya chini lengo likiwa ni kujadili changamoto zilizopo katika maeneo yao na kuzipatia ufumbuzi.
.jpeg)
.jpeg)

0 Comments