TANGAZO

TANGAZO

SINGIDA YATINGA NUSU FAINALI MAPINDUZI

 

Timu ya Singida Fountain Gate imefanikiwa kutinga nusu fainali Kombe la Mapinduzi baada ya kuiondosha Azam FC kwa kichapo cha mabao 2-1 mechi iliyochezwa katika Uwanja wa New Amaan, Zanzibar.

Mabao yaliyoipa ushindi Singida yamefungwa na Elvis Rupia dakika ya 62 na Habib Kyombo (65) huku bao pekee kwa Azam likifungwa na Alassane Diao (45).


Singida inasubiri mshindi kati ya Simba na Jamhuri ambao watashuka dimbani saa 2:00 usiku katika Uwanja wa New Amaan.

Post a Comment

0 Comments