TANGAZO

TANGAZO

TANROADS, TARURA KUKARABATI MIUNDOMBINU ILIYOHARIBIWA NA TOPE HANANG

  


Wakala wa Barabara Tanzania-TANROADS na Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini - TARURA, wameunganisha nguvu kukarabati miundombinu ya barabara katika Mji Mdogo wa Katesh, wilayani Hanang mkoani Manyara.

Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa, amewaambia waandishi wa Habari leo Desemba 06, 2023 kwamba, wameamua kuungana ili kuhakikisha mawasiliano ya barabara ikiwemo barabara kuu ya Babati - Singida inasafishwa ili safari ziendelee bila changamoto.

"Jana na leo hata nyie mnaona tofauti, mnaona watu wameanza kufungua maduka na kufanya biashara, haikuwa hivi na tunaamini wafanyabiashara wengi wataendelea kufungua maduka na biashara nyingine na hivyo kuruhusu maisha kuendelea," alisema Bashungwa na kuongeza:

"Baada ya kufungua barabara ikiwemo barabara kuu ya Singida - Babati tutahakikisha inapitika na kwa kushirikiana na Tanroads na Tarura tumetengeneza timu ya pamoja kusafisha barabara kubwa na zile za ndani."


Itakumbukwa kuwa Desemba 3, 2023, mvua kubwa iliyonyesha wilayani hapa na kusababisha maporomoko ya matope kutoka katika Mlima Hanang yaliyosababisha vifo vya watu 69, majeruhi zaidi 116, uharibifu wa mali na miundombinu.


Tanroads na Tarura, wanashirikiana na vikosi vya uokoaji ikiwemo Jeshi la Wananchi Tanzania-JWTZ pamoja na wananchi kuondoa tope lililojaa kwenye barabara, mitaro ya barabara na maduka yaliyopo pembeni mwa barabara.

Post a Comment

0 Comments