
Lakini kubwa zaidi nikuwa huwezi kumcontrol mpenzi wako anapokua mbali, humuoni hivyo huoni mambo anayoyafanya huko, anakua na uhuru wa kufanya chochote na nirahisi hasa kukusahau kuliko kama mngekua mnaishi karibu karibu.
Kama hutakua makini nirahisi kuharibu mapenzi yenu kwakua mnakosa ile ladha ya kuwa karibu. Lakini kama ukijua namna ya kuishi na mpenzi wako vizuri, bila kujali umbali aliopo, bila kujali ni muda gani amekua mbali unaweza kutengeneza mahusiano imara na hatua zifuatazo zitakusaidia kufanya hivyo.
(1) Anachofanya Huko Aliko Hakikuhusu; Nadhnai hiki ndiyo kitu kikubwa ambacho unapaswa kujifunza. Katika maisha kuna mambo ya aina mbili, aina ya kwanza ni yale mambo ambayo yapo ndani ya uwezo wetu, mambo ambayo tunaweza kuyabadili, kutawekea maamuzi.
Kwa mfano, wewe kuoga liko ndani ya uwezo wako, unaweza kuamua kuoga au kukaa na uchafu, wewe kufanya usafi, wewe kusoma, kuwa na tabia nzuri, kuheshimu watu, kuacha kuchepuka, kumtukana mwenza wako na mambo mengine kama hayo yako ndani ya uwezo wako.
Kwamba unaweza kuamua kuyafanya au kutokuyafanya. Lakini kuna mambo ambayo yako mbali kabisa nnje ya uwezo wako. Haya ni yale mambo ambayo huwezi kuyafanya wewe na yanafanywa na watu wengine. Kwa mfano, kupigwa na mumeo, kunyanyaswa na mkeo, kuachwa na mpenzi wako, kufukuzwa kazi.
Mambo haya yapo nnje ya uwezo wako kama ambavyo kile ambacho anakifanya mpenzi wako akiwa mbali na wewe kipo nnje ya uwezo wako. Kwamba wewe uko mbali, huwezi kumzuia kuchepuke, huwezi kumzuia asichelewe kurudi, huwezi kumlazimisha akupigie simu na mambo mengine mengi.
Sasa kama unataka kuwa na furaha ni kuchukua yale mambo ambayo yapo ndani ya uwezo wako na kuyafanya, lakini yale ambayo yako nnje ya uwezo wako ukamuachia Mungu. Sasa hembu acha kufuatilia kama mwenza wako akiwa mbali anafanya nini, anakua na nani, anatabia gani, anarudi nyumbani saa ngapi?
Hayo ni mambo ambayo hayakuhusu kwani kama huna mpango wa kumaucha, majibu utakayoyapata hayatatakusaidia kitu. Utagundua kweli anafanya mambo hayo lakini utazidi kuumia na kumchukia na ndiyo mwanzo wa kuachana, hivyo acha kufuatilia mambo anayoyafanya huko na jikite katika yale ambayo anayafanya mbele yako.
Kuna watu huharibu mahusiano yao kwa kutumia muda mwingi kuwachunguza watu wao huko waliko, waatafuta na walinzi kabisa, kujua kuwa ameingia saa ngapi, katoka saa ngapi, yuko wapi, na nani, anafanya nini na nini? Unapoteza muda kwani ukijua zaidi ya kulalamika hutafanya chochote hivyo hembu acha kujipa presha za bure.
(2) Namna Bora Ya Kuwasiliana Naye; Katika mapenzi ya mbali mawasiliano ndiyo kitu kikubwa ziadi, kupigiana simu na mpenzi wako, kuongea na kuambiana siku zenu ndiyo msingi mkubwa. Tatizo kubwa nikua watu hawajui namna ya kuwasiliana, kwamba mko mbali lakini mnatumia nusu au muda wote mnaozungumza kuzozana.
Kama mko mbali basi mara nyingi ni sababu ya kazi, inawezekana wote au mmoja wenu kaajiriwa au kajiajiri. Sasa hembu kuwamakini unapompigia mwenza wako simu, jua ratiba zake na jua muda wakazi, sio kwakua ni mumeo au mumeo ukadhani unaweza kumpigia kila saa, wasilianeno kwa siku kama mara tatu tu.
Isizidi sana kwani inaboa na isipungue sana kwani inaleta upweke. Fanyeni asubuhi, jioni na usiku, mida ambayo si ya kazi ili muweze kuongea vizuri bila vikwazo. Nyakati za kazi ni mbaya kwani mwenza wako anaweza kua na stress za kazi au wateja na wewe unataka kuongea, akakujibu vibaya ukakasirika na kuwamwazo wa migogoro.
Kitu mnachoongea pia ni muhimu, meseji mnazotumiana zinamanaa kubwa. Acheni kugombana au hata kutaka kutengeneza migogoro isiyo na maana, kwa mfano unampigia badala ya kumuambia kuhusu siku yako ilivyokua unaaanza kumuambia jana ulikua wapi, mbona hivi, mbona hukupokea mchana, mbona simu ilikua bize ulikua unaongea na wanawake/wanaume zako!
Kwamba wewe ni mtu wa kushutumu tu, mwanzo mwisho mwenza wako anasikiliza malalamiko yako. Nakuhakikishaia atakosa uvumilivu na ndiyi atakata mawaisliano kabisa, hakuna mtu anapenda kupoteza muda wake akiongea na mtu analalamika tu. Hembu ongeea kuhusu siku yenu, hata kama mlikorofishana.
Sahau kidogo, muambie kuhusu watoto, kuhusu maisha ya huko, mpige stori za mahaba ambazo hata hazieleweki, mpige na kaumbea kidogo. Yaani mpaka mtamaniane, muwe marafiki. Hapo hata atakumiss, atatamani kuongea na wewe kwakua unatia raha na si kualalamika lalamika na wivu wa kijinga jinga!
(3)Mambo Ya Kufanya Mnapoonana; Hatimaye sasa umeenda kumtembelea, au amekuja nyumbani. Badala ya kufurahia mahusiano yenu unaanza kufuatilia simu yake, kuangalia nani alikua anachat naye, kuangalia majirani, kujua nani kazoeana nae zaidi.
Lakini huishii hapo, unaanza kuchunguza kwa marafiki, kuona kama ana mtu anaingia ingia, yaani kwa kifupi baada ya mna muda umfurahie mwenza wako wewe ni kukumbushia maugomvi ya zamani, kufukunyua fukkunyua madhambi yake na kuanza kulalamika au kugombana.
Yaani mnaonana siku mbili lakini zinakua kero, anatamani hata uondoke kwani hana amani. Labda nikuambie kitu, haisaidii kitu kununua, hata kama antabia mbaya kama hataki hazibadiliki kwakua tu eti umenuna nuna, umejua na umetukana na hata kumpiga.
Kama humuamini mwenza wako kwasababu za kiafya hembu nendeni mkapime kwanza, ndiyo mfanye hayo mapenzi. Lakini sio unakuja siku mbili unagombana na kila mtu, kila rafiki, unaanza kukusanya umbea wote wa mambo aliyokua anayafanya. Huko ni kutafuta ugomvi usio na maana, kwamba mtagombana na siku za kukaa pamoja zitaisha na hamtafikia muafaka.
Lakini kwakua hamkufikiamuafaka basi hata ukiondoka, ukifika kwenye simu ni kugombana tena kuhusiana na kitu kile kile. Mwisho wa siku mnachokana, mnachukiana na mnaelekea kcuhana. Hivyo kama nilivyosema hapo juu, mambo ambayo yapo nnje ya uwezo wako, huwezi kuyacontrol hayo mauchia Mungu na muambie hili ni lako siliwezi.
Ukiyashika mambo haya mtatu, kwanza hutapata stress kila siku kuwaza anafanya nini? Pili utakua mtamu kuongea, kwamba mwenza wako yuko mbali lakini anatamani muda wenu wa kuongea ugefike muongee sio unapiga kila baada ya dakika tano na kutuma vimeseji vingi vingi ambavyo vinaboa, lakini mkiwa pamoja itakua raha kwani mnakua wapenzi na si hakimu na mtuhumiwa.
AHSANTEEEEE
0 Comments