TANGAZO

TANGAZO

Tazama Video : VYAMA VYA UPINZANI KAHAMA, VYAKIMBIZA MWENGE WA UHURU MSALALA







Baadhi ya Vyama vya upinzani wilayani Kahama (vyama rafiki), vimeungana na wananchi katika kuupokea na kushiriki katika mbio za mwenge wa Uhuru, uliobeba ujumbe wa '' Tanzania ni Yetu Sote, Tushikamane kwa pamoja kuleta Maendeleo.”



Vyama hivyo vimeshiriki katika kuukimbiza Mwenge wa Uhuru katika Halmashauri ya Msalala, mkoani Shinyanga, wakati mwenge huo ukihitimisha mbio zake katika halmashauri hiyo leo.



Ushiriki wa vyama vya upinzani katika mbio hizo, umeongeza sura ya ushirikishwaji wa makundi mbalimbali ya jamii katika shughuli zinazolenga kuhamasisha maendeleo, amani na mshikamano miongoni mwa Watanzania.



Katika safari yake Msalala, Mwenge wa Uhuru umepita katika maeneo mbalimbali ya halmashauri hiyo, ukiwa na ujumbe unaohamasisha wananchi kushiriki katika shughuli za maendeleo, kutunza mazingira na kutumia fursa zilizopo kwa ajili ya kuboresha maisha yao ikiwa ni dhamira ya Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan, ya kuhakikisha kila mtanzania anakuwa na maisha bora.



Ushiriki wa vyama vya upinzani katika kuukimbiza Mwenge huo unaelezwa kuwa sehemu ya kuonesha kuwa masuala ya maendeleo yanahitaji ushirikiano wa watanzania bila kujali itikadi za kisiasa.



Mwenge wa Uhuru unapoendelea na safari yake, wananchi wameendelea kupewa rai ya kudumisha amani, mshikamano na ushirikiano katika kujenga Taifa, huku viongozi na wadau mbalimbali wakisisitiza umuhimu wa kutunza miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa manufaa ya jamii.





Post a Comment

0 Comments