Idara ya Afya ya Afrika Kusini imewatahadharisha wananchi kuhusu ongezeko kubwa la wagonjwa wa rubella kote nchini humo hasa kutokana na kuripotiwa zaidi ya kesi 10,000 za watu walioambukizwa ugonjwa huo mwaka huu.
Taarifa hiyo imesema: “Kwa mujibu wa Taasisi ya Taifa ya Magonjwa ya Kuambukiza (NICD), jumla ya wagonjwa 10,137 wamegunduliwa nchini (Afrika Kusini) kati ya Januari na Novemba 2024, idadi ambayo ni kubwa kuliko kesi zilizorekodiwa mwaka jana.”
Taarifa hiyo imeongeza kuwa: “Kesi nyingi zimerekodiwa katika majimbo ya Gauteng na Cape Magharibi, wakati zaidi ya asilimia 90 ya kesi ni kwa watoto wa chini ya umri wa miaka 15.”
Rubella, ambao pia unajulikana kwa jina la “Surua ya Kijerumani,” ni ugonjwa wa virusi unaoambukiza sana lakini unaozuilika kwa chanjo.
Kwa mujibu wa Idara ya Afya ya Afrika Kusini, ugonjwa huo huenea kutoka kwa mtu hadi mtu mwingine kupitia makohozi au kupiga chafya hewani mgonjwa. Watoto na wanawake wajawazito wako katika hatari kubwa zaidi ya kuambukizwa ugonjwa huo wa rubella na madhara yake
C&P
0 Comments