TANGAZO

TANGAZO

TASAF YAJENGA KITUO CHA MABASI SONGEA

 


Na Said Mwishehe,Michuzi TV-Songea

MRADI wa Ujenzi wa Stendi ya mabasi unaotekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii(TASAF) katika Kijiji cha Lundusi wilayani Songea Mkoani Ruvuma umefika asilimia 78 huku wananchi wakieeleza kuwa Ujenzi huo itakapokamilika utaondoa changamoto ya usafiri pamoja na kuimarisha wa wananchi.

Kwa mujibu wa TASAF ni kwamba Matarajio Mradi huo inatakiwa uwe umekamilika Januari mwaka 2025 ili wananchi waanze kuonja matunda ya Stendi hiyo ambayo inakwenda kuondoa changamoto ya usafiri ambayo wananchi wa Kijiji hicho pamoja na Kata ya Peramiho na maeneo Jirani wamekuwa wakiipata kutokana na kutokuwa na Stendi ya mabasi.

Akizungumza kuhusu miradi ya TASAF inatotekelezwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma ikiwemo Mradi wa Stendi ya mabasi , Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Mwalimu Hassan Mtamba amesema ujenzi wa stendi hiyo unatakelezwa na TASAF na umelenga kuondoa changamoto ya usafiri kwa wananchi huku akitumia nafasi hiyo kumpongeza Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kwa jitihada zake za kusogeza huduma karibu na wananchi.

Mwalim Mtamba amesema kuwa wananchi wanataraji kuona mabasi makubwa kutoka maeneo mbalimbali yakifika mpaka Lundusi, na hivyo kuondoa adha ya usafiri kwa wananchi ikiwemo ya kutumia gharama kubwa wanapataka kusafiri.

“Kituo hiki cha mabasi kitakapokamilika na kuanza kutoa huduma kitawaondolea usumbufu na gharama wananchi wa maeneo hayo ambao kwa sasa inawalazi kuja mpaka Songea kupata huduma ya usafiri wa mikoani na maeneo mengine, tunaishukuru Serikali kupitia TASAF kwa kutupatia stendi hii.”

Kwa upande wake Mtendaji wa kijiji cha Lundusi, Imelda Mbawa amesema kuwa wananchi wa kijiji hicho na maeneo ya jirani wanapata shida wanapotaka kusafiri kwenda mikoani na maeneo mengine ambapo wanapaswa kusafiri kwenda Songea mjini kupanda mabasi.

Amefafanua wamekuwa wakitumia gharama kubwa sana, kwa mfano Mwananchi wa kijiji hicho anapotaka kwenda Dar es Salaam, Iringa au Mbeya,anatakiwa kuondoka kwenda kulala Songea ili kesho yake apande basi, hivyo stendi ikikamilika hatutakuwa na shida ya usafiri.

Awali  mwananchi wa kijiji hicho ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya ujenzi wa stendi hiyo, Henrik Haule ameeleza kuwa stendi hiyo ikikamilika itatoa fursa kwa wananchi hususani vijana na akina mama kufanya biashara na kujiongezea kipato.

Amesema wanaishukuru TASAF kwa kutuletea mradi huu wa ujenzi wa stendi,wanaamini uchumi wa wananchi utakuwa stendi hiyo ikikamilika na kuanza kufanya kazi huku akisisitiza vijana watapata fursa ya kufanya biashara.

Akizungumza kuhusu Mradi huo Mratibu wa TASAF Manispaa ya Songea, Hosana Ngunge amesema utekelezaji wa mradi huo wa stendi umetokana ma maombi ya wananchi wa kijiji hicho.

Amesema kuwa kasi ya Ujenzi wa Stendi hiyo inaridhisha na makubaliano yaliyopo Mradi huo unatakiwa uwe umekamilika Januari mwaka 2025 huku akieleza licha ya kuwa na mkandarasi anayeendelea na ujenzi pia kuna nguvu ya wananchi ambao wanafanya shughuli za ujenzi.

Wakati huo huo fundi kiongozi katika ujenzi huo, Peter Mashine amesema kuwa mpaka sasa ujenzi huo umefika asilimia 78 na unatarajiwa kukamilika Januari mwaka 2025 na kazi inaendelea kwa kasi inayoridhisha.

Mashine amesema ujenzi huu ulianza Agosti mwaka 2023 na utakapokamilika utakuwa na eneo la kuegesha mabasi, vyumba 36 vya biashara, matundu nane ya vyoo, jengo la utawala pamoja na jengo la ulinzi na usalama.













C&P.

Post a Comment

0 Comments