TANGAZO

TANGAZO

UWT YAWAONYA WABUNGE/MADIWANI WANAOWASAIDIA WALE TU WALIOWAWEZESHA KUKALIA NAFASI HIZO



Mwenyekiti wa UWT Taifa *Ndg. Mary Pius Chatanda* ametoa onyo kali kwa Waheshimiwa Wabunge na Madiwani wanaowasaidia wale tu waliowawezesha kukalia nafasi hizo.


Chatanda, ametoa onyo hilo Leo tarehe 20 Disemba, 2024 Mkoani Ruvuma akiwa ni mgeni rasmi katika hafla ya kugawa vitendea kazi mbalimbali ambazo ni mashine za kukamulia alizeti, vyerehani, majiko ya gesi, Ng'ombe wa maziwa, Baiskeli kwa mlemavu na Mifuko ya Saruji kwa makundi mbalimbali Mkoani Ruvuma.

Chatanda amepiga marufuku kwa Makatibu UWT Mikoa na Wilaya Wanaowatisha Wabunge ili wawapelekee zawadi ya pesa na vitenge jambo ambalo amesema ni kinyume na nafasi zao wanazozitumikia.

Katika hatua nyingine Mwenyekiti wa UWT Taifa amempongeza Mbunge Viti Maalumu Mkoani Ruvuma Mhe. Jackine Msongozi kwa kukumbuka makundi mbalimbali Mkoani humo hasa akina Mama

ambapo amewapatia vitendea kazi hivyo na kuwaasa Wabunge na Madiwani viti maalumu kuwa karibu na akina Mama kwani ndio waliowapatia nafasi hizo wanazozitumikia na kuwatafutia fursa mbalimbali na mikopo ya salama kwani ukimuwezesha mwanamke unakuwa umewezesha familia.

Ameendelea kutoa pongezi kwa Mhe. Jackline Msongozi Mbunge Viti Maalumu Mkoani Ruvuma kwa kutekeleza ilani ya CCM kwa vitendo kwa kuvipatia vikundi hivyo vitendea kazi na pia amemuunga mkono Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuinua akina Mama.

Amewataka wanawake Mkoani humo kutumia fursa hiyo kuongeza uzalishaji wa mazao mbalimbali ikiwemo Alizeti, Karanga, na Ufuta ambapo leo wamepatiwa mashine za kuchakata alizeti na kuongeza kuwa leo wamepokea vyerehani 700 mbali na vyerehani 500 ambavyo viliwahi kutolewa na Mbunge huyo.

Amewataka wanufaika kutunza vitendea kazi hivyo ili viwapatie manufaa.

Post a Comment

0 Comments