Chatanda ameyasema hayo Desemba 20,2024 alipokuwa mgeni rasmi katika hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Kanisa Katoliki la Bombambili, wilaya ya Songea Mjini, ambapo vifaa mbalimbali ikiwemo mashine za kukamulia alizeti, vyerehani, na mitungi ya gesiv yenye thamani ya jumla ya shilingi milioni 600 viligawiwa kwa makundi mbalimbali ya wanawake.
Mheshimiwa Chatanda amesema kuwa wanawake ni jeshi kubwa na muhimu linalotegemewa na taifa. Alisisitiza kuwa wanawake wanapaswa kuonyesha juhudi katika kupambana na kuleta maendeleo katika jamii, hasa wanapokabidhiwa majukumu makubwa.
Mbunge Msongozi amekabidhi mashine 20 za kukamua mafuta ya alizeti kwa vikundi 20, vyenye thamani ya shilingi milioni 400, vyerehani 700 vyenye thamani ya shilingi milioni 200, mitungi ya gesi 500, mifuko ya saruji kwa ajili ya uboreshaji wa nyumba za ibada (makanisa na misikiti), pamoja na ng'ombe wawili kwa wanavikundi wenye uhitaji wa kufuga mifugo.
Vifaa hivi vina lengo la kusaidia maendeleo ya jamii na kujenga umoja wa kujitolea miongoni mwa wananchi.
Wanawake wa vikundi walivyopokea vifaa hivyo wametoa shukrani kwa Mbunge Jacqueline Msongozi kwa upendo na msaada mkubwa aliowapatia.
Wameeleza kuendelea kujitolea kufanya kazi kwa bidii na juhudi, huku wakimwomba Mbunge huyo kuendelea kuwasaidia watu wengine ili waweze kujikwamua kiuchumi.
0 Comments