TANGAZO

TANGAZO

PICHA: MBUNGE NGAYIWA AHUDHURIA MAHAFALI YA 18 YA SHULE YA MSINGI SHUNU KAHAMA



Mbunge wa Jimbo la Kahama Mjini, Benjamin Ngayiwa, akiwa katika mahafali ya 18 ya Shule ya Msingi Shunu


NA NEEMA NKUMBI KAHAMA.


Mbunge wa Jimbo la Kahama Mjini, Benjamin Ngayiwa, amehudhuria mahafali ya 18 ya Shule ya Msingi Shunu iliyopo Manispaa ya Kahama, mkoani Shinyanga.


Katika mahafali hayo, jumla ya wanafunzi 197 wanahitimu masomo yao ya elimu ya msingi, kati ya wanafunzi 198 waliosajiliwa kufanya Mtihani wa Taifa wa Darasa la Saba katika shule hiyo.


Taarifa zinaeleza kuwa mwanafunzi mmoja kati ya waliosajiliwa kufanya mtihani huo ameshindwa kufanya mtihani kutokana na changamoto ya ugonjwa.


Mahafali hayo ni sehemu ya matukio yanayowakutanisha walimu, wazazi, walezi na wadau mbalimbali wa elimu katika kuadhimisha hatua ya wanafunzi kukamilisha elimu yao ya msingi.

PICHA 👇

Post a Comment

0 Comments