Msafara wa magari ya Kampuni ya MATI Super Brands LTD ukipita katika maandamano ya maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi) ngazi ya Mkoa wa Manyara. Picha na Malunde
Msafara wa magari ya Kampuni ya MATI Super Brands LTD ukipita katika maandamano ya maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi) ngazi ya Mkoa wa Manyara.
Wafanyakazi wa Kampuni ya MATI Super Brands LTD wakishiriki maandamano katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi) ngazi ya Mkoa wa Manyara

Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Mheshimiwa Queen Sendiga, akitembelea banda la Kampuni ya MATI Super Brands LTD wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi) ngazi ya Mkoa wa Manyara.
Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Mheshimiwa Queen Sendiga, akiangalia bidhaa za vinywaji katika banda la Kampuni ya MATI Super Brands LTD wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi) ngazi ya Mkoa wa Manyara. Kushoto ni Mkurugenzi wa Kampuni hiyo, David Mulokozi.
Mkurugenzi wa Kampuni ya MATI Super Brands LTD, David Mulokozi, akizungumza wakati Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Mheshimiwa Queen Sendiga, alipotembelea banda la kampuni hiyo katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi) ngazi ya Mkoa wa Manyara.
Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Mheshimiwa Queen Sendiga (kushoto), akiondoka katika banda la Kampuni ya MATI Super Brands LTD wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi) ngazi ya Mkoa wa Manyara. Katikati ni Mkurugenzi wa Kampuni ya MATI Super Brands LTD, David Mulokozi.

Mkuu wa Mkoa wa Manyara Queen Sendiga akikabidhi tuzo kwa Kampuni ya MATI Super Brands Ltd kwenye maadhimisho ya Mei Mosi 2026
Na Kadama Malunde - Malunde 1 Blog
Kampuni ya MATI Super Brands LTD yenye makao yake mjini Babati mkoani Manyara, ambayo ni kampuni mama ya MATI Foundation, MATI Zoo na MATI LTD South Africa, imeweka historia kwa kuvunja rekodi ya ushiriki katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani mwaka 2026 yaliyofanyika Mei Mosi 2026 katika Uwanja wa Tanzanite Kwaraa, Babati, ngazi ya Mkoa wa Manyara, baada ya kuingia na msafara mkubwa wa magari uliovutia hisia za wengi.
Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Mheshimiwa Queen Sendiga.
Katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani 2026 MATI Super Brands Ltd imeibuka mshindi wa kwanza kwa kutwaa tuzo katika vipengele vitatu, vikiwemo Tuzo ya Banda Bora la Maonesho pamoja na Ushindi wa Jumla wa Maonesho ya Mei Mosi Mkoa wa Manyara.
MATI Super Brands LTD ni wazalishaji wa vinywaji changamshi vya aina mbalimbali vinavyopatikana sokoni ndani na nje ya Tanzania, ikiwa ni moja ya makampuni yanayokua kwa kasi katika sekta hiyo.
Baadhi ya bidhaa zake kuu ni pamoja na Strong Dry Gin, Sed Cane Spirit, SED Pineapple Gin, Strong Coffee Potable Spirit pamoja na TAI Original Potable Spirit.
Vinywaji hivi vimejipatia umaarufu kutokana na ubora wake, ladha zake tofauti na upatikanaji wake mpana katika maeneo mbalimbali ya biashara.
Aidha, kampuni hiyo pia huzalisha bidhaa nyingine kama Tanzanite Premium Vodka, Tanzanite Royal Gin na Jax’s Will Premium Whiskey, ambazo zimeendelea kuimarisha nafasi yake katika soko la vinywaji changamshi.
MATI Super Brands LTD imejijengea heshima kama mzalishaji muhimu anayechangia ukuaji wa sekta ya viwanda na uchumi kupitia bidhaa zake zinazozalishwa kwa viwango vya ushindani.
Akizungumza katika maadhimisho hayo, Mkurugenzi wa MATI Super Brands LTD, Bw. David Mulokozi, ambaye ni mwekezaji wa ndani mzawa, amesema Tanzania ni eneo huru, lenye amani na salama kwa uwekezaji wa ndani na nje ya nchi.
Amesema mazingira mazuri ya biashara pamoja na fursa nyingi za kiuchumi zilizopo nchini yanaendelea kuwavutia wawekezaji katika sekta mbalimbali ikiwemo viwanda, utalii, kilimo na huduma.
Bw. Mulokozi ameweka bayana dhamira yake ya kuendelea kukuza uchumi wa Tanzania kupitia sekta za viwanda, utalii na hifadhi ya mazingira, huku akiwahamasisha wawekezaji wengine kutumia fursa zilizopo nchini kwa maendeleo ya taifa.
Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Mheshimiwa Queen Sendiga, amewapongeza wawekezaji wa mkoa huo akisema MATI Super Brands LTD ni mfano bora wa mwekezaji kutokana na mchango wake mkubwa katika maendeleo ya kiuchumi na kijamii.
Amesema kampuni hiyo imesaidia upatikanaji wa ajira kwa wananchi kwa kufungua nafasi nyingi za kazi, pamoja na kushiriki katika huduma za kijamii na kusaidia jamii inayowazunguka.
“Niwatie moyo wawekezaji wote wa Mkoa wa Manyara kwamba serikali itaendelea kuweka mazingira rafiki kwa wawekezaji ili kuinua uchumi wa wananchi. MATI Super Brands LTD wamekuwa wawekezaji wazuri katika mkoa wetu. Nimeona magari mengi leo kwenye maandamano, madereva wanaoendesha ni miongoni mwa wafanyakazi waliopata ajira katika kampuni hii,” amesema.
Aidha, amesisitiza kuwa serikali itaendelea kushirikiana na wawekezaji wenye nia njema ili kuchochea maendeleo ya Tanzania kwa ujumla.
Kwa sasa, MATI Super Brands LTD ni mwajiri wa wafanyakazi zaidi ya 1,000 nchini Tanzania pamoja na ukanda wa nchi za Maziwa Makuu na Afrika Kusini.
Sambamba na maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Uhuru wa Vyombo vya Habari na Siku ya Wafanyakazi Duniani, Bw. David Mulokozi na kampuni yake ya MATI Super Brands LTD wameonesha mshikamano na vyombo vya habari kwa kushirikiana na Chama cha Waandishi wa Habari Vijijini (RUJAT) ili kuhakikisha habari za vijijini pamoja na sauti za pembezoni zinapewa kipaumbele katika vyombo vya habari nchini Tanzania.


























































































0 Comments