Dar es Salaam – 05 Januari, 2025
Mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) unaotarajiwa kusafirisha mafuta kutoka Hoima nchini Uganda hadi Chongoleani mkoani Tanga, unaendelea kutoa manufaa makubwa ya kiuchumi kwa Tanzania na Uganda, hususan katika sekta ya ajira.
Akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari, Waziri wa Nishati wa Tanzania, Mhe. Deogratias Ndejembi, amesema mradi huo tayari umezalisha ajira 12,000 kwa vijana na wananchi wa Tanzania na Uganda, na utaendelea kutoa fursa zaidi kadri utekelezaji unavyoendelea.
Mhe. Ndejembi amesema hadi sasa utekelezaji wa mradi huo umefikia asilimia 79, na unatarajiwa kukamilika mwezi Julai mwaka 2026. Ameongeza kuwa kukamilika kwa mradi huo kutaiwezesha Tanzania na Uganda kusafirisha hadi mapipa 246,000 ya mafuta ghafi kwa siku.
Kwa upande wake, Waziri wa Nishati na Maendeleo ya Madini wa Uganda, Dkt. Ruth Nankabirwa, ameishukuru Serikali ya Tanzania chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa ushirikiano na dhamira ya dhati katika kuhakikisha mradi huo unatekelezwa kwa mafanikio.
Dkt. Nankabirwa amesema mradi wa EACOP umeleta mapinduzi makubwa ya kiuchumi katika ukanda wa Afrika Mashariki na kusisitiza umuhimu wa kutoa ajira kwa wananchi wa maeneo yanayopitiwa na mradi huo, sambamba na kuwajengea uwezo na ujuzi kwa miradi mingine ya baadaye.
Mradi wa bomba la mafuta ghafi una urefu wa kilomita 1,443, ambapo kilomita 296 zipo nchini Uganda na kilomita 1,147 zipo nchini Tanzania. Tanzania itakuwa na vituo vinne vya kusukuma mafuta, huku Uganda ikiwa na vituo viwili, hivyo kufanya jumla ya vituo sita













0 Comments