TANGAZO

TANGAZO

FAHAMU JINSI ABS SYSTEM INAVYOFANYA KAZI KWENYE GARI YAKO

 

Na Khalifa Hassan Simba 

Chuo cha Udereva ZITCO - KAHAMA 


➡️ANTILOCK BRAKING SYSTEM ..huu ni mfumo salama wa umeme unaoruhusu tyre kujidhibiti katika mpangilio wa mtetemo wakati dereva anapofunga brake..na kusababisha tyre kupunguza mwendo na kuepusha gari kukosa muelekeo....


➡️Kwa kawaida  unapokanyaga  brake nguvu ya uzito wa mwendo hukimbilia kwenye tyre za mbele asilimia 59.9.. na asilimia 39.9 kuwa kwenye tyre za nyuma....


*➡️Hivyo tyre za mbele huwa na brake zenye uwezo zaidi kuliko nyuma*


➡️Ushikaji wa brake ukitofautiana kati ya tyre ya kulia na kushoto ni tatizo...kwa kuwa lile lililoshika brake litakuwa linasota (skidding)  wakati ambalo halijashika brake litaendelea kutembea...


*➡️Kitendo cha tyre 1 kushika brake na lingine kutoshika kinawaeza kukuletea madhara makubwa kwani gari litavuta upande ulioshika brake na kama upo speed kubwa gari inaweza kupinduka*


NOTE:


*➡️Ukiwa speed kubwa na ukafunga brake ghafra..utahisi mtetemo kwenye pedal ya brake hapo ujue Abs system inafanya kazi sawia*


➡️vitu vinavyoweza kusababisha Abs system kutofanya kazi


1=kuharibika kwa Abs sensor


2=kuungua kwa fuse


3=kuharibika kwa Abs moter


4=Tatizo la wiring


Endapo kuna warning light ya Abs kwenye dashibody yako check kwa diagnosis machine kujua tatizo lilipo kiurahisi.

+255 767 040 022


MWISHO.

Post a Comment

0 Comments