TANGAZO

TANGAZO

RAIS MWINYI AZINDUA MAEGESHO YA GARI MALINDI

 
















Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inakusudia kujenga kituo cha kisasa cha mabasi ya abiria, pembezoni mwa maegesho ya gari Malindi, sambamba na ujenzi wa kituo kikubwa cha gari za abiria pamoja na kiwanja cha michezo kwa vijana.



Rais Dk.Mwinyi ameyasema hayo alipofungua maegesho ya gari ya kwanza ya ghorofa Malindi Zanzibar, Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi ikiwa ni shamrashamra za miaka 61 ya Mapinduzi ya Zanzibar.



Aidha Rais Dk. Mwinyi amesema Serikali itaendelea kutekeleza ujenzi wa  miradi mengine mikubwa ya kimkakati inayotarajiwa ukiwemo  mradi wa taxi za baharini ambapo ujenzi wa bandari za taxi hizo umeanza Maruhubi zitakazosafirisha na kushusha abiria watakaotumia usafiri wa majini kwa kutumia taxi hizo, ujenzi wa treni zitakazotumia barabara za lami kutoka Malindi mjini hadi Bububu, ujenzi wa barabara nne za juu zenye mapishano pamoja na ujenzi wa jeti kwa usafiri wa baharini kuwasafirisha watalii wanaotembelea visiwa vidogovidogo.




Kwa upande mwingine , Rais Dk. Mwinyi ameupongeza Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar, ZSSF kwa kutekeleza wajibu wao wa kutoa mafao kwa wananchi kwa wakati na kwa kiwango kizuri, kuwekeza kwenye miradi yenye tija na kufanikiwa kutoa mchango kwa maendeleo ya nchi kwa kujenga miradi mikubwa, akitolea mfano mataifa mengine duniani kuwa mifuko ya hifadhi ya jamii ndio inayojenga nchi, hivyo aliitaka ZSSF kuendeleza utaratibu huo.


Vilevile Rais Dk. Mwinyi  amewasisitiza wananchi kuendelea kudumisha amani ya nchi, umoja na mshikamano ili nchi iendelee kupiga hatua kubwa za maendeleo.


Post a Comment

0 Comments