TANGAZO

TANGAZO

KESI ZA UBAKAJI, ULAWITI ZINAONGEZEKA - TAWJA

 


CHAMA Cha Majaji Wanawake (TAWJA) kimesema kesi za ubakaji na ulawiti zinaongezeka kwa kasi katika mikoa yote nchini na kwamba hali hiyo imekuwa tishio katika jamii.



Akizungumza jana Desemba 19,2024 wakati wa kuelekea maazimisho ya miaka 25 ya TAWJA,Mwenyekiti wa chama hicho ambaye pia ni Jaji wa Rufani Barke Sehel amesema miongoni mwa changamoto wanazokutana katika uendeshaji kesi ambapo miongoni ni ongezeko kubwa la kesi za ubakaji na ulawiti.

" Hivi sasa katika kila mkoa kunakua na kesi za ubakaji na ulawiti ,wakati kwa kipindi cha nyuma kulikua na mikoa baadhi tu iliyokua imekithiri na inayojulikana kwa kesi hizo,na chama hicho kinafanya jitihada za kuhakikisha zinatatuliwa lakini pia elimu inatolewa kwenye masuala ya usawa wa kijinsia,"amesema Sehel.

Amesema kwa sasa kila mkoa kumekuwa na kesi hizo za ubakaji na ulawiti tofauti na miaka ya nyuma ambayo kesi hizo zilikuwa kwa kwenye baadhi ya mikoa hivyo hali iliyopo sasa inasikitisha.

Akizungumzia kuhusu TAWJA amesema maadhimisho ya miaka 25 yanasherehekea mafanikio makubwa yaliyofikiwa katika maeneo hayo.

Amesema jamii inasherehekea mchango ya TAWJA katika usawa wa kijinsia ndani ya mfumo wa Mahakama na juhudi zake za kuboresha haki za wanawake na makundi dhaifu.

“Hadi sasa, mafanikio ya TAWJA yanatufanya tuzingatie maendeleo yaliyofikiwa na kazi endelevu inahitajika ili kuendeleza mfumo wa kisheria wenye usawa na unaojumuisha wote,” amesema.

Naye , Jaji Mstaafu wa Mahakama Kuu ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya maadhimisho hayo, Sophia Wambura amesema katika kipindi cha miaka 25,TAWJA imefanikiwa kukuza hali ya usawa kwenye ngazi ya utendaji wa Mahakama.

"Vilevile tumehamasisha usawa kwenye jamii katika kuijengea uwezo kutambua haki zao katika mirathi, talaka na haki za usawa na masuala mengine ya kijamii,” amesema.

Hata hivyo Jaji wa Mahakama Kuu kanda ya Arusha na mwenyekiti wa kamati mwenyeji ya maandalizi ya maadhimisho hayo, Aisha Bade amesema bado kuna changamoto za dhamana.

Amesema pamoja na kwamba dhamana zinakua wazi lakini wahusika wanashidwa kutimiza masharti ya dhamana kwa kukosa baadhi ya mahitaji kama mdhamini na vitambulisho, jambo ambalo katika maadhimisho hayo pia watatoa elimu hiyo.




 

Post a Comment

0 Comments