Naibu Waziri Mkuu ambaye pia ni Waziri wa Nishati Dkt. Dotto Biteko katika hafla hiyo ya kuukaribisha mwaka 2024, amewataka watanzania kudumisha Umoja na mshikamano ili kuepuka chuki zinazoenezwa na watu wenye nia ovu zinazoweza kuvuruga amani hasa kulelekea kipindi cha Uchaguzi.
‘’Watu wa Mbogwe, tunaposherehekea
mwaka 2024, nitoe wito nilioutoa kwa watu wa Bukombe kwa sababu nyinyi ni watu
wa jamii moja ‘’Tuvumiliane’’ mwaka 2024 fanya kazi moja ya kumfanya mtu mmoja
kuwa na furaha katika Maisha yake, kama kuna mtu amekukosea mwaka 2024 fanya
kazi ya kumsamehe, kama kuna mtu amekutendea wema fanya kazi ya kumshukuru, kuwa
na ibada ya kutenda wema kwa jirani yako, umpende kama unavojipenda wewe mtoto
wa mwenzio mlee kama wa kwako, ukiona mwenzio ana tatizo, likuhusu na likuume
kama tatizo lako, mkifanya hivyo mtafanya ibada iliyo njema, na mtaifanya kuwa
Mbogwe ya watu wanaothaminiana na kupendana, mkifanya hivyo maendeleo mtayaona’’
Alisema
‘’Rais wetu Dkt Samia
Suluhu Hassan amefanya kazi kubwa ya kuwaunganisha watanzania, kwa vyama na
dini na makabila mbalimbali, anataka wote tuimbe kama watanzania wa kundi moja,
na sisi wasaidizi wake tumebeba ujumbe wa Dkt. Samia Suluhu Hassan’’
‘’Jamani Watanzania Rais
tulie nae amewaweka Watanzania kwenye Daraja linalofanana amesikiliza
malalamiko yao, wa vyama vya upinzani walivyolalamika akawaita, akasema
nawafungulieni nendeni mkafanye mikutano mueleze sera zenu, wamekuja kwenu n
ahata hapa wamekuja tena kwa vyombo tofauti tofauti, wamekuja kwa magari
wamekuja kwa helkopta, wamepewa fersa hiyo na serikali yetu ya kuwasaidia
watanzania waweze kuzungumza yale wanayoona yanawafaa kwa maslahi ya nchi yetu,
amefanya hivyo ili kujenga mshikamano na umoja kwa Watanzania’’
‘’Tutakuwa na uchaguzi
mwaka huu wa serikali za mitaa kama uchaguzi huo, tuutumie kutafuta viongozi
walio bora, kama kuna kiongozi anafanya kazi nzuri kama Maganga kwenye mtaa
wako, mumuunge mkono mumchague, na mumpe nafasi ya kuongoza tena, kama kuna
kiongozi mnaona anaweza kurekebishwa, mrekebisheni hapa sasa ivi mpaka wakati
wa Uchaguzi na mumpe nafasi ya kuongoza tena’’
‘’Utakuja uchaguzi
utahusisha vyama vingine vya upinzani na chama tawala kamwe watu wa Mbogwe
msigawanyike kwa kutukanana kwa sababu tu ya uchaguzi, kwa sababu baada ya
uchaguzi kutakuwa na maisha yanaendelea’’
‘’Muutumie huu uchaguzi kuzungumza matatizo yenu, shida yam aji, Barabara, umeme, shida ya Watoto wetu kuwa na mahali pa kusomea, mzungumze yale yanayowaunganisha kama wana-Mbogwe na msiruhusu mtu yoyote kuja kuwagawanya na kuwafundisha chuki katikati yenu’’ Alisema Naibu Waziri mkuu Doto Biteko alipokuwa akizungumza na wakazi wa Mbogwe katika Hafla hiyo ya kuukaribisha mwaka 2024
Mbunge wa Jimbo la Mbogwe Mkoani Geita, Mhe. Necodemus Maganga akizungumza.
Baadhi ya wananchi wa wilaya ya Mbogwe wakiwa katika Hafla ya kuukaribisha mwaka 2024.
0 Comments