TANGAZO

TANGAZO

MAGARI MABOVU NA DEREVA AMBAYE HAJAHAKIKI LESENI YAKE MARUFUKU BARABARANI - SACP. NG'ANZI


Na Mwandishi Wetu

Kamanda wa Kikosi cha usalama barabarani Nchini, SACP. Ramadhani Ng'anzi amesema kuwa gari lolote bovu halitaruhusiwa kupita barabarani huku Madereva ambao leseni zao hazijahakikiwa hawataruhusiwa kuendesha Magari barabarani.

Kamanda Ng'anzi ametoa kauli hayo Disemba 16,2023 katika maeneo ya Mwandege mkoa wa Kipolisi Rufiji wakati akizungumza na waandishi wa habari amesema hatua hiyo ni kukabiliana na kudhibiti ajali za barabarani zinazopelekea Vifo na majeruhi.


Na kuongeza kuwa Jeshi la Polisi nchini linafanya operesheni endelevu nchi nzima ya ukaguzi wa magari yote ili kuyabaini magari mabovu, kuwapima ulevi madereva, kukagua ujazaji wa abiria kwenye magari, kukagua mikanda ya magari, kukagua leseni za madereva kama zimehakikiwa, kukagua kama abiria wote wana tiketi mtandao na pia kuangalia manifesti yenye kulingana na idadi ya abiria waliopo kwenye basi.



Katika operesheni hii kamanda amebainisha wazi kuwa mabasi 15 yalikaguliwa katika ya hayo mabasi 5 yalibainika kuwa ni mabovu yalizuiliwa kuendelea na safari, wamiliki, mawakala na madereva walielekezwa kuyapeleka magari gereji kwa matengenezo.


Kamanda Ng'anzi alikagua leseni za madereva wa magari ili kuwabaini madereva ambao hawajahakiki leseni zao ambapo madereva saba (7) walinyang'anywa leseni zao kwani madereva hawa wanaendesha magari bila kuhakiki leseni zao.



Katika operesheni hii Kamanda aliwapima madereva ulevi ili kujiridhisha kuwa madereva wanaoendesha magari barabarani hawana kiwango cha ulevi mwilini. Matokeo ya upimaji ulevi ni kwamba hakuna dereva aliyebainika kuwa na kilevi mwilini.

Halikadhalika, Kamanda huyo alifanikiwa kukagua madeni kwa magari ya mabasi, malori na magari madogo, hakuna aliyekuwa anadaiwa deni kutokana na makosa ya usalama barabarani.

Kamanda wa Kikosi cha usalama barabarani ametoa wito kwa wakuu wote wa usalama barabarani nchini (RTOs) kufanya ukaguzi wa kina wa magari na wasiruhusu magari mabovu kuendeshwa barabarani, pia wasiruhusu basi kuzidisha abiria na wakiyabaini basi abiria hao washushwe na watafutwe usafiri mwingine.

Pia, amewataka RTOs wote kusimamia mwendo kasi wa magari katika himaya zao, na wasimamie madereva wasiwe Wana overtake hovyo kwenye sehemu zisizoruhusiwa au maeneo ambayo ni hatarishi na watakaowabaini wawakamate, wawaweke mahabusu na wawafungulie mashtaka na wawafikishe mahakamani.


Katika operesheni hiyo Kamanda aliambatana na Mkuu wa Usalama barabarani Kanda maalum, ACP. William Mkonda, RPC mkoa wa Kipolisi Temeke, ACP. Malulu, Mkuu wa usalama barabarani mkoa wa Temeke, SP. SULE na Mkuu wa usalama barabarani mkoa Rufuji, ASP. Manyama akiwemo pia DTO Wilaya ya Mbagala, ASP.
Mwakyonike pia DTO wilaya ya Mkuranga, Insp. Hamidu, halikadhalika alikuwemo A/insp Polycarp, wakaguzi wa magari watatu (3) na askari wa R&F 15 walishiriki katika Operesheni. Operesheni hii ilikuwa ni muunganiko (JOII) kati yaya Maafisa toka Trafiki kuu, Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Wakuu wa Usalama barabarani wa mikoa miwili ya kipolisi ya Temeke na Rufuji.

Post a Comment

0 Comments