TANGAZO

TANGAZO

Tazama video - MAHONA CUP-12' YAANZA SAFARI YA KUMSAKA MSHINDI WA MILIONI TANO NA KOMBE





Mechi ya ufunguzi ni kati ya Itinde U20 Fc na Luton Fc, zote kutoka kata ya Segese katika Halmashauri ya Msalala, wilayani Kahama, mkoani Shinyanga.


Mechi hiyo imechezwa katika uwanja wa shule ya msingi Segese, huku mgeni rasmi akiwa ni mwenyekiti wa CCM Kata ya Segese Peter Hassan.


Akizungumza muda mfupi kabla ya kuanza kwa mchezo huo, Hassan ameziasa timu zote mbili kushiriki kwa kufuata kanuni, taratibu na sheria zote za mchezo wa soka ili kuleta matokeo yanayotarajiwa.


Amesema “Ninaziasa timu zote kuwa tulivu na kushiriki michezo hii kwa kufuata sheria zote zinazosimamia mchezo wa soka, lakini pia michezo hii itumike kuhamasishana kuhusu masuala ya ulinzi na usalama kwa kushirikiana na mamlaka zilizopo.”


Nae muasisi wa ‘Mahona Cup’ Patrick Mahona amesema ligi hiyo kwa mwaka 2026, msimu wa 12 umelenga kuwaandaa vijana kushiriki katika timu za ligi kuu kwa watakaochaguliwa.


Amesema “Mashindano haya yameibua vipaji na wapo vijana ambao wametoka katika ligi hii na wamesajiliwa katika timu zinazoshiriki ligi kuu, daraja la kwanza na la pili.”


ZAWADI

Amefafanua kuwa mshindi wa kwanza sasa atapata zawadi ya fedha taslimu shilingi milioni tano (5,000,000) pamoja na kombe, mshindi wa pili atapata fedha taslimu shilingi milioni 2.5, mshindi wa tatu atapata shilingi laki tano na wa nne kusalia na mipira miwili.


Mchezaji bora, mfungaji bora pamoja na kijana atakayecheza akiwa na umri mdogo zaidi atapata zawadi.


HATUA YA MTOANO

Mechi ya ufunguzi Agosti 26, 2026 ni kati ya Itinde Fc na Luton Fc, Agost 27, 2026 ni kati ya Supertiger Fc na Chemichemi Fc. Agost 28, 2026 ni kati ya Kilimanjaro Fc na Imani Academy, Agost 29, 2026 ni kati ya Mlimani Fc na Newboys Ntobo. Agost 30, 2026 ni kati yam AHONA Boys na Veterans Fc.


ENDELEA KUTUFUATILIA…..




 

Post a Comment

0 Comments