TANGAZO

TANGAZO

NDEJEMBI AAPISHWA KUWA MAKAMU WA RAIS


Makamu wa Rais, Deogratius Ndejembi, ameapishwa rasmi kushika wadhifa huo leo, Agosti 29, 2026, katika hafla iliyofanyika Ikulu ya Chamwino, jijini Dodoma.


Ndejembi ameapishwa na Jaji Mkuu wa Tanzania, George Masaju, huku Rais Samia Suluhu Hassan na viongozi mbalimbali wa Serikali wakishuhudia tukio hilo.

Uteuzi wa Ndejembi unafuatia jina lake kupendekezwa Agosti 26, 2026 na Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa (NEC), kuziba nafasi iliyoachwa wazi na Dk. Emmanuel Nchimbi, aliyejiuzulu na baadaye kufukuzwa uanachama wa CCM.

Jana, Agosti 28, 2026, jina la Ndejembi liliwasilishwa Bungeni na kuthibitishwa kwa kura 329 za ndiyo, sawa na asilimia 100 ya wabunge waliokuwepo.

Post a Comment

0 Comments