TANGAZO

TANGAZO

BALOZI MBAROUK ASEMA ITALIA INA NAFASI KUBWA YA KULETA WATALII NCHINI




📌Aipongeza Wizara Ya Maliasili na Utalii kutangaza fursa za utalii nje ya nchi


📌Jaji Mruma naye atembelea Banda la Maliasili kujionea wanyamapori hai Nane Nane


Na Neema Chalila Mbuja, Dodoma

BALOZI wa Tanzania nchini Italia na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO), Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD) na Shirika la Chakula la Umoja wa Mataifa (WFP), Mhe. Mbarouk Nassoro Mbarouk leo Agosti 04, 2026, ametembelea Banda la Wizara ya Maliasili na Utalii na kusema kuwa nchi ya Italia ina nafasi kubwa ya kuleta watalii wengi nchini.


Mhe. Balozi Mbarouk amesema Tanzania inafanya vizuri kwenye kutangaza utalii na vivutio vyake na kuipongeza Wizara kwa kazi nzuri inayoifanya.


Katika hatua nyingine Wizara ya Maliasili na Utalii imepokea ugeni wa Jaji wa Mahakama ya Rufaa Mhe. Rajab Mruma ambaye ameitaka Wizara ya Maliasili na Utalii kubuni mbinu za kutafuta utatuzi wa changamoto za wanyamapori hai kuingia kwenye makazi ya wananchi kwa kujenga uzio ili kuzuia uharibifu unaoweza kutokea.


Aidha, Mhe Jaji Mruma ametembelea bustani ya wanyamapori hai iliyoko kwenye Maonesho ya Nane Nane yanayoendelea Jijini Dodoma ikiwa ni sehemu ya kutangaza utalii wa ndani kwa wananchi.








Post a Comment

0 Comments