MAZINGIRA bora ya uwekezaji yanayofanywa na Serikali katika sekta ya nishati ya mafuta na gesi imeendelea kuwa kichocheo cha kuvutia wawekezaji na hivyo kusogeza upatikanaji wa nishati hizo karibu na wananchi.
Kauli hiyo imetolewa leo Juni 15,2026 jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mkuu wa Oryx Energies Tanzania Limited Iman Mtafya wakati wa uzinduzi wa kituo kipya cha Oryx kilichopo Wazo ambapo amesema lengo la kuzinduliwa kwq kituo hicho ni kusogeza huduma za nishati ya mafuta pamoja na nishati safi ya kupikia ya gesi karibu na wananchi.
“Oryx ndio tunaongoza kwenye usambazaji wa gesi na tutaendelea kuiunga mkono serikali katika kuhamasisha nishati safi.Uzinduzi wa kituo hiki ni kusogeza huduma zetu katibu na wananchi na tunamtandao mpana wa vituo sehemu mbalimbali nchini.
“Kwahiyo tunaendelea kuwekeza maeneo mbalimbali na tumeanza hapa na hivi karibuni tutafungua kituo kingine ambacho kitakuwa umbali wa kilometa 40 kutoka Dodoma Mjini.Lengo ni kuonesha kama kampuni tunaendelea kuwafikia wateja kokote walipo, hata vijijini.”
Akieleza zaidi kampuni ya Oryx inajali usalama na katika kituo hicho wametumia teknolojia ya juu huku akisisitiza katika bidhaa zao wanajali bora kwani ni kampuni ambayo wanayo maabara ya kupima obora wa bidhaa zao ili kuhakikishia wateja mafuta wanayoweka katika vyombo vya moto yamezingatia ubora.
Mtafya amesema pia kama Serikali inavyoendelea kuweka mazingira bora ya uwekezaji ndio maana unaona tunaendelea kukua na sio hapa tu Dar es Salaam bali na mikoani.
“Mazingira yaliyowekwa na Serikali kupitia Wizara ya Nishati wawekezaji tunapata msaada mkubwa wa kupanua wigo wa kusogeza huduma karibu na wananchi, katika sekta ya nishati tunaona Waziri wa Nishati anavyoendelea kuhamasisha uwekezaji katika sekta ya nishati .
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa CDT Oil na CDT Energies Boniphace Nasibu ambaye ndio msimamizi wa kituo hicho katika biashara ya mafuta,vilainishi pamoja na gesi amesema wameangalia jami inayozunguka eneo hilo na kuona kuna kila sababu ya kusogeza huduma.
“Kituo chetu kipo karibu Madale ambako kuna mashamba ya jeshi,kiwanda cha saruji cha Wazo pamoja na watu wa eneo la Wazo na kwa ujumla tumejiridhisha hapa ni sehemu sahihi ya kuwahakikishia wananchi kupata mafuta na gesi ya kupikia.”
Amewahakikishia wateja wao watapata huduma zote zinazostahili ili wafurahie huduma za Oryx zinazopatikana huku akiishukuru oryx kwa kufanikisha uwepo wa kituo hicho.
Wakati huo huo akizungumza kwa niaba ya wananchi wa eneo la Wazo Sheikh Amani Hamis amesema kufunguliwa kwa kituo hicho mbali ya kusogeza huduma za nishati ya mafuta pamoja na gesi pia imewezesha vijana wa eneo hilo kupata ajira kupitia kituo hicho.
0 Comments