TANGAZO

TANGAZO

RAIS SAMIA ATOA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KIFO CHA MWIGIZAJI HASHIM KAMBI



Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametuma salamu za rambirambi kufuatia kifo cha mwigizaji mkongwe wa filamu nchini, Hashim Kambi, kilichotokea leo jijini Dar es Salaam.

Kupitia salamu zake, Rais Samia amesema amepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo hicho, akieleza kuwa Taifa limepoteza kipaji adhimu kilichochangia kwa kiasi kikubwa kukuza na kuitangaza tasnia ya filamu nchini.

Aidha, Rais Samia ametoa pole kwa Shirikisho la Filamu Tanzania, Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA), wasanii wa filamu nchini pamoja na familia ya marehemu, ndugu, jamaa, marafiki na wadau wote walioguswa na msiba huo.

“Inna lillahi wa inna ilayhi raji'un,” amesema Rais Samia katika salamu zake za pole.

Marehemu Hashim Kambi anakumbukwa kwa mchango wake mkubwa katika tasnia ya filamu nchini, ambapo alijizolea heshima kutokana na kazi zake zilizogusa maisha ya Watanzania wengi.

Post a Comment

0 Comments