Mtuhumiwa wa mauaji hayo anatajwa kuwa mgeni ambaye bado hajafahamika aliyefika nyumbani kwa marehemu majira ya saa 3:00 usiku wa Aprili 3, 2026 na kula pamoja na marehemu chakula sambamba na wajukuu wa marehemu kabla ya marehemu kumsindikiza mtu huyo kwa ajili ya kumpeleka kwa mtalaamu wa tambiko la kuzuia kutapata watoto pacha.
Hata hivyo inaelezwa kuwa muda mchache baada ya wawili hao kutoka mieni alirejea nyumbani hapo na kurejesha tochi kisha kuwataarifu wajukuu wa marehemu kuwa ‘bibi huyo atarejea asubuhi kutoka kwa mganga ambaye ni mama yake mdogo’.
Taarifa iliyotolewa anaeleza kuwa mwili wa marehemu uligundulika baada ya mjukuu wa marehemu aliyekuwa akielekea shambani asubuhi kubaini uwepo wa damu nyingi na nguo za marehemu kisha kuwafahamisha ndugu wa marehemu ambao baada ya kufuatilia waliukuta mwili wa marehemu ukiwa umetupwa shambani ukiwa umekatwa mapanga shingoni.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, SACP Janeth Magomi, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa uchunguzi wa awali inaonesha kuwa chanzo cha mauaji hayo ni imani za kishirikina na tayari watu wawili wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

0 Comments