SPIKA wa Bunge, Mussa Azzan Zungu (Mb), anawatangazia Wabunge kwamba, vikao vya Kamati za Kudumu za Bunge vimeahirishwa kwa siku ya Machi 25, 2026 kufuatia kifo cha William Vangimembe Lukuvi (Mb), aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Watu Wenye Ulemavu) na Mbunge wa Jimbo la Isimani.
Shughuli hizo za Kamati zinaahirishwa kwa mujibu wa Kanuni ya 176 ya Kanuni za Kudumu za Bunge Toleo la Agosti, 2025.
Lukuvi amefariki asubuhi ya leo Machi 25, 2026 katika Hospitali ya Benjamin Mkapa alipokuwa akipatiwa matibabu.


0 Comments