Wananchi wa Kata ya Lunguya iliyopo Halmashauri ya Msalala mkoani Shinyanga wamehimizwa kushirikiana kwa karibu na Jeshi la Polisi pamoja na vikundi vya Sungusungu ili kuhakikisha vitendo vya uhalifu vinakomeshwa na kudumisha amani na usalama katika maeneo yao.
Wito huo umetolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Janeth Magomi, alipokuwa akizungumza na wananchi wa kata hiyo katika mkutano uliofanyika Lunguya.SACP Magomi amesema kuwa usalama ni jukumu la kila mmoja, na kwamba Jeshi la Polisi haliwezi kufanya kazi hiyo peke yake bila ushirikiano wa wananchi pamoja na vikundi vya ulinzi shirikishi kama Sungusungu.Ameeleza kuwa Sungusungu ni wadau muhimu katika kuhakikisha usalama katika jamii, lakini wanapaswa kufanya kazi zao kwa kuzingatia sheria, taratibu na kushirikiana kwa karibu na Jeshi la Polisi ili kuepuka kujichukulia sheria mkononi.“Tunawahimiza wananchi kutoa taarifa za uhalifu mapema, kushirikiana na Sungusungu na Polisi, na kuepuka kuwaficha wahalifu kwani kufanya hivyo kunahatarisha usalama wa jamii nzima,” amesema SACP Magomi.




0 Comments