Katika mwendelezo wa kuwajengea uwezo wafanyabiashara wa ndani kupitia mafunzo yanayotolewa na kampuni ya Barrick nchini kupitia Programu yake ya kuendeleza biashara za ndani ili ziweze kunufaika na sekta ya madini (Local Business Development Programme), Wajasiriamali wapatao 150 kutoka wilaya za Msalala, Kahama na Nyang’hwale, wanapatiwa mafunzo ya biashara ya wiki mbili ambayo yamefunguliwa na Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Mboni Mhita.
Mafunzo haya ambayo yanafanyika katika hoteli ya Kitapela, yanayotolewa na wataalamu mbalimbali wa masuala ya kibiashara yamelenga kuwawezesha wajasiriamali waliopo katika maeneo yanayozunguka mgodi wa dhahabu wa Barrick Bulyanhulu kuweza kuchangamkia fursa za kibiashara na kunufaika na uwekezaji wa mgodi huo sambamba na kupata maarifa zaidi ya kuendesha biashara zao kitaalamu.
Katika hotuba yake ya ufunguzi, Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Mboni Mhita, aliipongeza Barrick Bulyanhulu kwa kuendesha mafunzo hayo na kuwataka washiriki kutoka kata tatu zinazozunguka Mgodi wa dhahabu wa Barrick Bulyanhulu, kuchangamkia fursa za mikopo ya asilimia 10, inayotolewa halmashauri zote ili kujikwamua kiuchumi.
“Mnaoshiriki mafunzo kupitia program hii muyazingatie kikamilifu ili muweze kuwa na vigezo vya kuchangamkia biashara zilizopo mgodini na kupata ujuzi wa kufanya biashara zenu kwa weredi nje ya mgodi”, alisema Mhita.
Kaimu Meneja Mkuu wa Mgodi wa Barrick Bulyanhulu,Victor Lule, alisema Kampuni ya Barrick inaamini kwamba msingi wa maendeleo ndani ya jamii unatokana na watu na hatua sitahiki kwenye fursa zinazopatikana ndio sababu ya kuwekeza katika programu hii ili kuwahamasisha kuzitambua fursa hizo.
Aidha alisema Mgodi wa Barrick Bulyanhulu unajivunia kuona idadi kubwa ya washiriki wa mafunzo hayo wanatokea katika kata mbalimbali jirani na mgodi ambao watanufaika na mafunzo yanayotolewa kupitia program hii ili waweze kuchangamkia fursa za kibiashara mgodini sambamba na kukuza biashara zao.
Mafunzo hayo yanaendeshwa na washauri wabobezi wa masuala ya kibiashara kutoka sekta ya umma na binafsi, ambapo yanatarajiwa kuwaongezea wafanyabiashara hao ujuzi, maarifa, mbinu na uwezo wa kubaini fursa mpya za kibiashara ndani na nje ya nchi ili kuweza kufikia malengo yao - wakizingatia vigezo, masharti, sheria na kanuni za Serikali na Kampuni ya Barrick ambayo inaendesha shughuli zake nchini kwa ubia na Serikali ya Tanzania kupitia kupitia Kampuni ya Twiga Minerals.
Tangu Programu hii ianzishwe tayari imewafikia wafanyabiashara mbalimbali waliopo maeneo jirani na migodi ya Barrick North Mara na Bulyanhulu na yamewawezesha baadhi yao kuchangamkia fursa migodini na kupata mafanikio makubwa ya kibiashara.
Akiongea kwa niaba ya washiriki wa mafunzo, Anastazia Ibrahim, kutoka Nyang’hwale, alisema matarajio yao ni kupata ujuzi utakaowawezesha kuchangamkia fursa za kibiashara zinazojitokeza sambamba na kuendesha biashara zao kitaalamu na kufuata sheria za nchi.
Kaimu Meneja Mkuu wa Mgodi wa Barrick Bulyanhulu,Victor Lule akiongea wakati wa hafla wa uzinduzi wa mafunzo hayo.
Mkufunzi wa mafunzo hayo Siraji Nalikame kutoka kampuni ya Impacten akitoa Mfunzo kwa washiriki
MenejaMahusiano na Mazingira wa mgodi wa Barrick Bulyanhulu,Agapit Paul akiongea na washiriki wa mafunzo hayo
Mkufunzi Rashidi Mwakatuma kutoka Impacten akitoa mafunzo kwa Washiriki wa Mafunzo haya.
Mkufunzi kutoka Jukwaa la Uwezeshaji wananchi kiuchumi Wilaya ya Kahama, Jozaka Bukuku akitoa mada kwenye mafunzo hayo.
Washiriki na wafanyakazi wa Barrick Bulyanhulu wakifuatilia matukio wakati wa uzinduzi
Washiriki na wafanyakazi wa Barrick Bulyanhulu wakifuatilia matukio wakati wa uzinduzi
Washiriki na wafanyakazi wa Barrick Bulyanhulu wakifuatilia matukio wakati wa uzinduzi
Makundi mbalimbali ya washiriki na wafanyakazi wa Barrick Bulyanhulu katika picha ya pamoja na mgeni rasmi wakati wa uzinduziMakundi mbalimbali ya washiriki na wafanyakazi wa Barrick Bulyanhulu katika picha ya pamoja na mgeni rasmi wakati wa uzinduzi
Makundi mbalimbali ya washiriki na wafanyakazi wa Barrick Bulyanhulu katika picha ya pamoja na mgeni rasmi wakati wa uzinduzi
0 Comments