TANGAZO

TANGAZO

ZAIDI YA WANAFUNZI 130 WALIOTEKWA NIGERIA WAACHILIWA


Wazazi wakiwa wanasubiri taarifa juu ya watoto wao waliotekwa katika shule ya Kuriga nchini Nigeria, Machi 9, 2024

 Zaidi ya wanafunzi 130 waliotekwa na watu wenye silaha katika shule moja kaskazini magharibi mwa Nigeria mapema mwezi huu wameachiliwa hii leo bila ya kujeruhiwa, maafisa na jeshi wamesema.

Msemaji wa jeshi Meja Jenerali Edward Bubaateka amesema waliookolewa ni wanawake 76 na wanaume 61. Amesema waliokolewa katika Jimbo la Zamfara na watakabidhiwa kwa Serikali ya Jimbo la Kaduna kwa hatua zaidi.

Ofisi ya gavana wa jimbo la Kaduna imesema watu hao wameachiliwa siku chache kabla ya muda wa mwisho wa kulipa dola 690,000 za kikomboleo zilizodaiwa na watekaji.

Gavana wa Kaduna Uba Sani amesema Mshauri wa Usalama wa Taifa nchini humo ndiye aliyeratibu kuachiliwa kwa wanafunzi hao, bila ya kutoa maelezo zaidi.

Tukio hilo la kuwateka wanafunzi 287 la Machi 7 lilikuwa la kwanza lililohusisha idadi kubwa ya watu tangu mwaka 2021, wakati zaidi ya wanafunzi 150 walipotekwa katika shule moja ya sekondari ya Kaduna.


Post a Comment

0 Comments