Na Mwandishi Wetu ,Manyara.
Chama cha Wafanyabiashara wenye Viwanda na Kilmo Mkoa wa Manyara (TCCIA Manyara) kimekanusha taarifa zilizosambaa mitandaoni zikimtaja mshauri wa biashara na mwajiriwa wa TCCIA Manyara Bw. Ramadhani Rashid Msangi kuhukumiwa kwenda jela miaka 3 au kulipa faini ya shilingi 900,000 kwa kosa la kughushi nyaraka za mafunzo kwa wajasiriamali mwaka 2018 hukumu iliyotolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Manyara tarehe 23 March 2024. Ambapo Chama hicho kimedai kuwa licha ya tuhuma zinazomkabili Bw.Ramadhani Rashid Msangi, kwa sasa sio mwajiriwa wa Chama hicho kwani aliondolewa kazini tangu April 2019 .
Taarifa kwa vyombo vya habari imetolewa na Uongozi wa Chama hicho ikieleza kuwa Mfanyakazi huyo aliondolewa miaka kadhaa iliyopita na tangu wakati huo hahusiki na shughuli zozote za Chama hicho. Chama Chetu TCCIA, kinaendelea kufanya kazi kwa uwazi na kwa kufuata sheria na taratibu zilizowekwa katika katiba yetu.
Tunajitahidi kufuata miongozo na mifumo iliyoainishwa katika katiba yetu, pamoja na kuzingatia sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Tunathamini uwazi na uwajibikaji katika kazi zetu, na tunajitahidi kuhakikisha kwamba tunazingatia viwango vya juu vya maadili na utawala bora katika kila hatua tunayochukua.(Mwenyekiti TCCIA Manyara)
0 Comments